TIMU YA COMBINE YA UMISSETA YATAKIWA KUYATUMIA MASHINDANI YA COPA COCACOLA AFRIKA KAMA FURSA YAO YA MAISHA NA MAENDELEO YA MICHEZO NCHINI.

Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Alex Nkenyenge amewataka wachezaji wa timu ya Taifa ya Umisseta ijulikanayo kama ‘Combine’ kuyatumia mashindano ya Afrika ya Copa Coca Cola kama fursa ya maisha na maendeleo ya michezo nchini, timu inayoenda kwenye mashindano yajulikanayo kama COPA AFRICA CUP yanayotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 08 hadi 16 Disemba, 2018 Mjini Nairobi nchini Kenya.
Rai hiyo ameitoa leo tarehe 07 Disemba 2018, wakati wa hafla ya kuikabidhi bendera timu hiyo ya Umisseta inayojumuisha wachezaji kutoka Mikoa ipatayo 8 ya Tanzania waliochaguliwa katika mashindano ya Umisseta na Umitashumta yalifanyika mwezi june mwaka huu Jijini Mwanza.
“Yatumieni mashindano haya kama fursa yenu nyingine ya maisha lakini pia ya maendeleo ya michezo nchini,”aliwaeleza Nkenyenge.

Aidha, Nkenyenge amewataka kuhakikisha kuwa wanaitumia fursa waliyoipata vizuri kwa kuiwakilisha nchi kwa ushindi na Watanzania wako pamoja nao kwa maombi waweze kufanya vizuri na kuwasisitiza kuwa wasiwaangushe.
Kwa upande wake Kocha wa timu hiyo na Mwalimu wa Sekondari ya Kibasila Abel Amon Mtweve ameeleza kuwa, timu yake ameindaa vizuri na wachezaji wake vizuri kwahiyo watanzania wawe na Imani kuwa watarudi na ushindi.
Timu ya Umisseta Copa Coca Cola inawakilishwa na wachezaji 16 akiwemo Nahodha Bashiru Twalib, Said Noshad, Mahmud Kassim, Hemed D. Benjemin, Adam John, Omary S. Muhawi na Thabith T. Siogopi kutoka Dar es salaam, Lameck Y. Mkuli na Elisha N. Malugu kutoka Mwanza, Luqman Juma kutoka Dodoma, Sadick Mdoe kutoka Tanga, Marco J. Kilowoko kutoka Tabora, Edgar H. Masebo kutoka Mbeya, Hassan S. Seleman na Ramia J. Abdallah kutoka Morogoro, na Shomary H. Mussa kutoka Kagera.
56 total views, 1 views today