AZANIA .A. MABINGWA WA MASHINDANO YA BASEBALL TAIFA 2018.

Mashindano ya sita (6) kitaifa kwa mchezo wa Baseball na Softball 2018, yamefikia tamati leo 09 Disemba, 2018 kwa timu ya Azania A kutoka wa Dar es Salaam kuibuka Bingwa wa mashindano hayo baada ya kuinyuka timu ya Sanya juu kutoka mkoani kilimanjaro katika mchezo wa fainali uliopigwa katika uwanja wa Baseball Koshien uliopo katika shule ya Sekondari Azania jijini Dar es Salaam.

IMG_2065

Akizungumza wakati wa ufungaji wa mashindano hayo, mwakilishi wa mgeni rasmi kutoka shirika la mashirikiano ya kimataifa kutoka nchini Japan (JICA), Ndugu Kimura amewapongeza wachezaji pamoja na waalimu wao wote walioshiriki katika mashindano hayo kwa kufanikisha kumalizika kwa mashindano hayo sanjari na kuwapongeza pia wafanyakazi mbalimbali wa kujitolea kutoka Shirika la JICA ambao wamekuwa msaada mkubwa kama makocha katika mashindano hayo.

IMG_2236

“niwapongeze sana wachezaji pamoja na waalimu wenu wote mlioshiriki katika mashindano haya kwa kufanikisha kumalizika kwa mashindano lakini pia niwapongeze pia wafanyakazi mbalimbali wa kujitolea kutoka Shirika la JICA ambao wamekuwa na msaada mkubwa kama makocha katika mashindano haya,”Alisema Kimura.

IMG_2239

Aidha Kimura amesema kuwa JICA kwa muda mfupi limefanikiwa kuwakusanya baadhi ya wafanyakazi wake wa kujitolea kutoka Fukuoka Kyoiku Daigaku pamoja na kuusambaza mchezo wa Baseball katika shule za msingi wilaya ya Temeke tangu mwaka uliopita.

 

109 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by EmailO
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/12/09/azania-a-mabingwa-wa-mashindano-ya-baseball-taifa-2018/">
RSS