MAKATA KUKIONGOZA TaBSA KWA AWAMU NYINGINE TENA

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limesaidia kuratibu na kusimamia uchaguzi wa Chama cha mchezo wa Baseball na Softball Tanzania (TaBSA) Tarehe 9 Disemba 2018 katika ukumbi wa shule ya Sekondari Azania Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa TaBSA Neema Msitha akitangaza matokeo baada ya uchaguzi, pembeni kulia ni makamu mwenyekiti wa  uchaguzi Milinde Mahona na kushoto ni Katibu Mkhutasi wa uchaguzi TaBSA Maisara Mlambalazi wakisikiliza kwa makini matokeo ya uchaguzi yaliyokuwa yanasomwa na mwenyekiti.
Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa TaBSA Neema Msitha akitangaza matokeo baada ya uchaguzi, pembeni kulia ni makamu mwenyekiti wa uchaguzi Milinde Mahona na kushoto ni Katibu Mkhutasi wa uchaguzi TaBSA Maisara Mlambalazi wakisikiliza kwa makini matokeo ya uchaguzi yaliyokuwa yanasomwa na mwenyekiti.

Katika uchaguzi huo, Ndugu Ahmedi Makata ndiye alipewa ridhaa na wapiga kura ya kukiongoza TaBSA kama mwenyekiti kwa Awamu nyingine ya miaka minne baada ya kupata kura 10 za ndiyo na 0 ya hapana ikiwa ni mgombea pekee katika nafasi hiyo.

Abdul Kher Mohamed aliteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti kwa kupata kura 9 za ndiyo na 1 ya hapana kutoka kwa wajumbe baada ya kugombea nafasi hiyo pekeake hivyo kuingia katika nafasi hiyo kwa mara ya kwanza, huku kwa upande wa nafasi ya Katibu Mkuu Ndugu Alpherio M. Nchimbi ameibuka kidedea kwa kupata kura 10 za ndiyo na 0 ya hapana baada ya kuwa mgombea pekee katika nafasi hiyo.

IMG_2038
Katibu Mhutasi wa kamati ya uchaguzi wa TaBSA, Maisara Mlambalazi akiwa anagawa karatasi za kupigia kura kwa wajumbe na wapiga kura wakati wa zoezi la uchaguzi lililofanyika katika ukumbi wa Azania Sekondari Jijini Dar es Salaam.

Upande wa nafasi ya Katibu Mkuu Msaidizi Mwajibu S. Chingwaru alishinda nafasi hiyo kwa kupata kura 6 akimshinda Hussein A. Suleiman aliyepata kura 4 kati ya kura 10 zilizopigwa na wajumbe, huku nafasi ya Mhazini ikitakiwa kujazwa katika kipindi cha mwaka mmoja baada ya kukosa mgombea katika nafasi hiyo.

Nafasi za Wajumbe waliochaguliwa ni pamoja na nafasi ya mjumbe mwakilishi Baseball ambapo mgombea Haruni Rashid amepata kura 9 za ndiyo na 1 ya hapana, katika nafasi ya mjumbe mwakilishi Softball, Marcel S. Nkodeya amepata kura 10 za ndiyo na 0 ya hapana huku katika nafasi ya Mkurugenzi Ufundi Softball, Ndugu Gerald Hezwa amepata kura 10 za ndiyo na 0 ya Hapana na nafasi ya Mkurugenzi ufundi Baseball imechukuliwa na Musa Mbugi aliyepata kura 10 za ndiyo na 0 ya hapana.

IMG_2024

Mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi toka Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Neema Msitha ameupongeza uongozi mpya na kuutaka uongozi huo kuhakikisha wanaziba nafasi ambazo hazipata wagombea ndani ya mwaka mmoja, ili kukifanya chama hicho kuwa hai katika utendaji wake wa kazi katika Nyanja zote.

“Napenda kuupongeza sana uongozi mpya uliochaguliwa kuingia madarakani, ila tu niwaombe kwa zile nafasi ambazo bado hazijazwa mzijaze nafasi ndani ya kipindi cha mwaka mmoja, ili kuhakikisha kuwa chama kinafanya vizuri katika nyanja zote za utendaji kazi wake bila kuwa na matatizo yoyote ya kiuongozi,”alisema Neema.

IMG_1878

Nae Mwenyekiti wa TaBSA Dokta Ahmedi Makata ameushukuru uongozi wa BMT kwa kusimamia vyema uchaguzi huo na kuahidi kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa na Baraza sambamba na kuwataka viongozi waliochaguliwa kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha kuwa shughuli za TaBSA zinasimamiwa na kuendelezwa ipasavyo.

IMG_2267

“Naushukuru sana Uongozi wa BMT kwa kusimamia vyema uchaguzi huu na tunahaidi kuwa tutatekeleza maelekezo yote tuliyopewa na Baraza na pia niwaombe viongozi wote tuliochaguliwa tufanye kazi kwa bidiii ili kuhakikisha kuwa shughuli za TaBSA zinasimamiwa na kuendelezwa ipasavyo,”Alisema Makata.

2,117 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by EmailO
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/12/09/makata-kukiongoza-tabsa-kwa-awamu-nyingine-tena/">
RSS