UCHAGUZI WA YANGA KUFANYIKA MWEZI JANUARI KAMA ILIVYOPANGWA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt. Harrison G. Mwakyembe amesema kuwa tarehe ya uchaguzi wa viongozi wa klabu kongwe nchini Yanga bado ipo palepale kwa nafasi zilizotangazwa kujazwa licha ya kuwa na sintofahamu kwamba kuna baadhi ya viongozi na wanachama wanataka uchaguzi huo ufanyike kwa nafasi nyingine na sio nafasi ya Mwenyekiti kwani bado wanamtambua Bwana Yusuf Manji kuwa ndio mwenyekiti wa klabu.

IMG_2495Mheshimiwa Mwakyembe ameyasema hayo tarehe 17 Disemba, 2018, alipokuwa anazungumza na waandishi wa Habari ambapo amesema wamekuwa wakifanya vikao na viongozi wa klabu ya Yanga, Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF) pamoja na viongozi wa Serikali kuhusu mustakabali wa uchaguzi wa klabu hiyo na sasa wamekubaliana kuwa klabu hiyo inahitaji uongozi bora, imara wenye kuwajibika kwa wanachama wake kikamilifu na wenye kuheshimu katiba ya Yanga na hivyo kuleta tija katika Soka la Nchi.

“tumekuwa tukifanya vikao na viongozi wa klabu ya Yanga, TFF pamoja na viongozi wa serikali kuhusu mustakabali wa uchaguzi wa klabu ya Yanga na tumekubaliana kuwa klabu hii inahitaji uongozi bora, Imara wenye kuwajibika kwa wanachama wake kikamilifu na kuheshimu katiba ya Yanga, hivyo kuleta tija katika soka la nchi,” alisema Mh. Mwakyembe.

IMG_2574Aidha Mheshimiwa Mwakyembe amesisitiza kuwa zoezi la uchaguzi wa Yanga litasimamiwa na kamati ya uchaguzi ya TFF baada ya kamati ya uchaguzi klabu ya Yanga kushindwa kusimamia uchaguzi huo katika awamu zilizopita, hivyo na kuona ni vyema sasa TFF ikasimama kidete kuhakikisha kuwa uchaguzi unafanyika na klabu ya Yanga inapata viongozi bora.

IMG_2549“nashukuru sana tumekaa meza moja na viongozi wa Yanga wanaoongoza klabu hivi sasa kuhusu suala la nani atasimamia uchaguzi wa Yanga, tumewaomba kuwa uchaguzi usimamiwe na kamati ya uchaguzi ya TFF kwa sababu kamati ya klabu ya Yanga ilishapewa nafasi hiyo na ilishindwa kusimamia uchaguzi kwa sababu haukufanyika, ni vyema sasa TFF ikasimama kidete kuhakikisha kuwa uchaguzi unafanyika na klabu ya Yanga inapata viongozi bora,”alisema Mh.Mwakyembe.

844 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email5
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/12/17/uchaguzi-wa-yanga-kufanyika-mwezi-januari-kama-ilivyopangwa/">
RSS