MAJINA NANE YA WATU WANAOIVURUGA KLABU YA YANGA YAFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA USALAMA

Serikali kupitia Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo nchini, Yusuph Singo imetaja majina ya watu nane wanachama wa klabu kongwe nchini Yanga wanaodaiwa kuihujumu klabu hiyo kwa kuwakwamisha uchaguzi mkuu ambao umepangwa kufanyika 13 Januari, 2018.

IMG_2762Akitoa taarifa hiyo kwenye vyombo vya habari kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison G. Mwakyembe, Mkurugenzi Singo amesema Waziri amepokea majina ya watu hao ambao wamekuwa wakifanya vikao vingi vya siri ili kuhakikisha kuwa wanaivuruga Amani iliopo katika klabu hiyo na hivyo taarifa zao zimefikishwa katika vyombo vya usalama kwa ajili ya uchunguzi zaidi na endapo watakutwa na hatia, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

“Ndugu waandishi wa Habari Mheshimiwa Waziri amepokea majina ya watu ambao wamekuwa wakifanya vikao vya siri kuvuruga uchaguzi wa klabu ya yanga ambao umepangwa kufanyika mwezi January Mwakani, majina hayo yamefikishwa katika vyombo vya usalama kwa ajili ya uchunguzi na endapo kama watabainika kuwa na hatia, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao,”alisema Singo.

Aidha Singo amesisitiza kuwa, tayari Serikali imetoa kauli ya mwisho kuhusu Uchaguzi wa Klabu ya Yanga, ambao baadhi ya wanachama wa klabu hiyo wamekuwa wakipinga na kusema kuwa hawautambui uchaguzi huo kutokana na kusimamiwa na TFF huku wakisisitiza kuwa wanaendelea kumtambua Mwenyekiti wao Yusuf Manji.

Majina ya watu hao yaliyowekwa hadharani ni pamoja  Mustapha Mohammed, Edwin Kaisi, Said Bakari Lunguno (Mosha), Shaban Omary Mgonja(Uda), Kitwana Kondo Kipwata, Boaz Ikupilika Kipingo, Bakiri Makere na David Sanare.

 

1,608 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email5
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/12/19/majina-nane-ya-watu-wanaoivuruga-klabu-ya-yanga-yafikishwa-katika-vyombo-vya-usalama/">
RSS