BMT LATANGAZA MFUMO MPYA WA MALIPO KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limetangaza utaratibu mpya wa malipo yote yanayofanyika katika akaunti za Taasisi hiyo kwa kutumia mfumo wa kielectroniki wa kutumia kumbukumbu namba ijulikanayo kwa jina la (Control number).

IMG_2862Akizungumza na vyombo vya habari leo tarehe 27 Disemba, 2018, Afisa Habari wa BMT Najaha Bakari amesema Baraza limeanza kutumia mfumo huo wa kieletroniki kukusanya mapato ya Serikali kwenye makusanyo yake yote kwa Wadau wake vikiwemo Vyama/Mashirikisho na Vilabu vya Michezo.

Aidha, Afisa Najaha amesema mteja anapotaka kufanya malipo yoyote, afike ofisini au afanye mawasiliano kwa namba 0735 414043 au 0735 892889 ili kupata maelekezo sahihi, Vile vile mteja anaweza kutumia mojawapo kati ya barua pepe zifuatazo:  oscar.zablon@nationalsportscouncil.go.tz au alinanuswe.mwamundela@nationalsportscouncil.go.tz ili kupata namba ya utambulisho wa malipo husika (Payment Control Number) kabla ya kufanya malipo.

 1. Malipo yanaweza kufanywa kwa njia ya kibenki kwa kufuata hatua zifuatazo;
 2. Anapopata kumbukumbu ya malipo (Control Number);
 3. Tembelea Tawi lolote la Benki ya NMBna NBC;
 • Baada ya kuwasili benki na kumpa mtoa huduma wa dirishani namba ya kumbukumbu ambapo, mchakato wa malipo utakamilishwa.
 1. Lakini pia, malipo yanaweza kufanyika kwa njia ya mtandao wa simu ya mkononi kwa kutumia (M-pesa, Tigo Pesa na Airtel Money) kwa kufuata hatua zifuatazo;
 2. Kupitia simu yako, piga *150*00#, au *150*01# au *150*60#;

(Kupitia M- pesa, Tigo Pesa na Airtel Money);

 1. Chagua ‘Lipia malipo (Pay-Bills)’;
 2. Chagua ‘Malipo ya Serikali’;
 3. Chagua ‘Ingiza namba ya malipo’ na kuingiza namba ya kumbukumbu ya malipo (Control Number);
 4. Weka kiasi cha fedha unachotaka kulipa;
 5. Thibitisha muamala wako kwa kuingiza neno au namba yako ya siri; na
 6. Hifadhi ujumbe uliopokea katika simu yako unaoeleza ‘Malipo yamepokelewa National Sports Council’ kama ushahidi wa malipo endapo utahitajika kuonesha.

 

2,063 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email5
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/12/27/bmt-latangaza-mfumo-mpya-wa-malipo-kwa-njia-ya-kielektroniki/">
RSS