BMT LAENDELEA KUBORESHA NA KUDUMISHA USHIRIKIANO NA VYAMA VYA MICHEZO NCHINI

Baraza la michezo la Taifa (BMT) limeendelea na mpango wake wa kufanya Ziara ya kutembelea vyama na mashirikisho ya michezo kwa lengo la kutambua changamoto, kujadiliana Programu za maendeleo ya michezo sanjari na kuboresha, kudumisha ushirikiano baina ya BMT na vyama vya Michezo nchini.

IMG_3087

Akizungumza na viongozi wa kamati ya Olimpiki Tanzania alipowatembelea ofisini kwao tarehe 10 Januari 2019, kaimu Kaimu Katibu Mkuu wa BMT, Neema Msitha amesema ni utaratibu ambao Baraza umejiwekea Tangu mwaka 2018, kutembelea vyama na mashirikisho ya michezo nchini kwa lengo la kuboresha na kudumisha ushirikiano ili kupiga hatua katika maendeleo ya michezo nchini.

“ndugu viongozi wa TOC huu ni utaratibu ambao BMT umejiwekea tangu mwaka jana kutembelea Ofisi za vyama na mashirikisho ya michezo nchini kwa lengo la kuboresha na kudumisha ushirikiano ili kuhakikisha tunapiga hatua katika maendeleo ya michezo nchini, lakini pia kufahamu changamoto mnazokabiliana nazo ili kuweza kusaidiana kimawazo jinsi ya kujikwamua” alisema Neema.

Aidha Afisa Neema amesema Tanzania inajiandaa kushiriki katika mashindano makubwa ya Michezo ya Afrika “all African games” itakayofanyika mwaka 2019 pamoja na michezo ya Olimpiki 2020 itakayofanyika Tokyo Japani hivyo ni vyema vifanyike vikao vya maandalizi baina ya BMT, TOC na vyama vya michezo husika katika mashindano hayo.

“kama tunavyofahamu ni kwamba Tanzania inajiandaa kushiriki katika mashindano makubwa ya Michezo ya Afrika “All African Games” itakayofanyika mwaka 2019 pamoja na michezo ya Olimpiki 2020 itakayofanyika Tokyo Japani hivyo ni vyema tukafanya vikao vya maandalizi kati yetu na kamati ya Olimpiki na vyama vingine vya michezo husika katika mashindano haya”alisema Neema.

IMG_3112

Kwa upande wake Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Gulam Rashid amesema ni vyema sasa Baraza lione uwezekano wa kuanzisha tuzo za Michezo ili kutoa motisha kwa wanamichezo wanaofanya vizuri katika mashindano ya kitaifa na kimataifa.

“ndugu wajumbe wa kikao hiki, mimi kwa maoni yangu ninaona sasa ni wakati muafaka Baraza lione uwezekano wa kuanzisha tuzo za michezo ili kuweza kutoa motisha kwa wanamichezo wanaofanya vizuri katika mashindano ya kitaifa na kimataifa, na kwa kupitia hili tutaweza kupata wanamichezo wazuri na wenye ushindani zaidi” alisema Gulam.

 

 

75 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email5
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2019/01/10/bmt-laendelea-kuboresha-na-kudumisha-ushirikiano-na-vyama-vya-michezo-nchini/">
RSS