KANUNI ZA NGUMI ZA KULIPWA ZAPITISHWA, TAREHE YA UCHAGUZI MKUU KUTANGAZWA HIVI KARIBUNI.

Wadau wa mchezo wa ngumi za kulipwa nchini, wamepitisha kanuni zitakazotumika katika mchezo huo, baada ya kuandaliwa na viongozi wa kamati ya mpito ya kusimamia ngumi za kulipwa, kuzipitia kipengele kwa kipengele kwa takribani muda wa saa tano (5) na kufikia maamuzi ya kuzipitisha kanuni hizo huku ikisubiriwa kutangazwa tarehe ya uchaguzi wa kamisheni hiyo ili kuweza kupata viongozi wapya.

Waziri mwenye dhamana ya michezo nchini Mheshimiwa Dokta Harrison G Mwakyembe akifungua mkutano wa kuzipitia kanuni za kusimamia ngumi za kulipwa Tanzania, uliofanyika katika moja ya kumbi za uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Waziri mwenye dhamana ya michezo nchini Mheshimiwa Dokta Harrison G Mwakyembe akifungua mkutano wa kuzipitia kanuni za kusimamia ngumi za kulipwa Tanzania, uliofanyika katika moja ya kumbi za uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Akifungua mkutano wa kuzipitia kanuni hizo waziri mwenye dhamana ya michezo nchini Mheshimiwa Dokta Harrison G Mwakyembe, ameipongeza kamati ya kusimamia ngumi za kulipwa kwa kazi nzuri waliyoifanya kuandaa katiba pamoja na kanuni za kusimamia ngumi pamoja na kusaidia kuendesha uchaguzi mkuu wa kamisheni hiyo unaotarajiwa kufanyika kabla ya mwezi wa nne (4) mwaka 2019.

“ndugu waandishi wa habari na wadau wa ngumi za kulipwa mliokusanyika hapa, kwanza kabisa napenda kuipongeza kamati ya kusimamia ngumi za kulipwa kwa kazi nzuri waliyoifanya kuandaa katiba pamoja na kanuni za kusimamia ngumi ambazo leo mnazipitia kanuni, na kanuni hizi zikishapita basi tutakuwa tunasubiri kufanya uchaguzi huru ili kuweza kupata uongozi wa kudumu ili ngumi za kulipwa ziweze kurejesha heshima yake hapa nchini” alisema Dkt. Mwakyembe.

IMG_3165

Naye Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Makoye Alex Nkenyenge kabla ya kumkaribisha Mheshimiwa Waziri amesema BMT limekuwa karibu sana na kamati ya mpito kuisaidia kuiandaa katiba pamoja na kuisajili sanjari na kuziandaa kanuni za kuendesha ngumi za kulipwa.

“Mheshimiwa waziri kabla sijakukaribisha kuzungumza na wadau wa ngumi za kulipwa niseme tu kwamba tumekuwa karibu sana na kamati ya mpito ya kusimamia ngumi za kulipwa nchini ambapo tumeshirikiana kuhakikisha wanaandaa katiba ambayo tayari tumeshaisajili na leo wanamalizia kuzipitia kanuni ambazo zitapelekea kufanyika uchaguzi ambao utatupatia viongozi wapya wa kuindesha kamisheni kwa uweledi na uwezo mkubwa” alisema Nkenyenge.

469 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email5
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2019/01/11/kanuni-za-ngumi-za-kulipwa-zapitishwa-tarehe-ya-uchaguzi-mkuu-kutangazwa-hivi-karibuni/">
RSS