BMT LAKAGUA MIUNDOMBINU YA BAADHI YA SHULE ZINAZOFUNDISHA ELIMU KWA MICHEZO NCHINI.

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limeanza ziara ya kutembelea na kukagua miundombinu ya shule zinazofundisha elimu kwa michezo katika mikoa ya Pwani, Dar es Salaam, Lindi, Mtwara na Morogoro kwa lengo la kuandaa mkakati mahususi wa uboreshaji wa shule hizo.

IMG_3285Akizungumzia suala hilo akiwa katika shule ya Morogoro Sekondari, Afisa maendeleo ya Michezo kutoka BMT, Milinde Lutiho Mahona amesema Serikali kupitia Wizara ya Habari, Wizara ya TAMISEMI na Baraza la Michezo la Taifa, imeamua kufanya ukaguzi huo kwa lengo kuu la kufanya tathmini ya utekelezaji wa shughuli za michezo na ufundishaji wa elimu kwa michezo katika maeneo ya miundombinu, vifaa vya michezo pamoja na walimu wenye taaluma ya michezo.

IMG_3333“Serikali imeona umuhimu wa michezo nchini kwani michezo ni Afya na ni ajira pia, hivyo imeamua kufanya ukaguzi kwa shule ambazo zinafundisha elimu kwa michezo ili kufanya tathmini ya utekelezaji wa shughuli za michezo na ufundishaji katika maeneo ya miundombinu,vifaa vya michezo pamoja na walimu wenye taaluma ya michezo ili tuweze kuandaa mkakati mahususi wa uboreshaji wa shule hizi” alisema Mahona.

IMG_3250Kwa upande wake Afisa Michezo Mkoa wa Morogoro Bi. Grace Njau ameipongeza Serikali kwa hatua nzuri iliyochukua ya ukaguzi wa shule zinazofundisha Michezo, kwani kuna vijana wengi sana wenye vipaji ambao wakipata miundombinu bora na vifaa vya michezo wataweza kuongeza juhudi na kuwa wachezaji bora katika michezo mbalimbali nchini na kuweza kulisaidia Taifa katika mashindano mbalimbali ya kimataifa.

IMG_3323“kwa kweli niipongeze sana serikali kwa hatua nzuri waliyoichukua ya kukagua shule zetu ambazo zinafundisha elimu kwa michezo, kwani naamini hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kuweza kuongeza Ari kwa wachezaji kufanya vizuri Zaidi na kulisaidia Taifa katika mashindano mbalimbali ya kimataifa katika siku za usoni” alisema Grace.

Mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Morogoro Sekondari Hussein Msumbiji akielezea changamoto katika usomaji wa somo la Elimu kwa Michezo.
Mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Morogoro Sekondari Hussein Msumbiji akielezea changamoto katika usomaji wa somo la Elimu kwa Michezo.

Nao baadhi ya wanafunzi wa Morogoro Sekondari wamelezea changamoto kubwa wanayokabiliana nayo katika kusoma somo la Elimu kwa Michezo kuwa ni miundombinu mibovu pamoja na ukosefu wa vifaa kwa baadhi ya michezo wakati wa kusoma somo hilo kwa vitendo.

441 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email5
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2019/01/16/bmt-lakagua-miundombinu-ya-baadhi-ya-shule-zinazofundisha-elimu-kwa-michezo-nchini/">
RSS