MHESHIMIWA MWAKYEMBE AMPONGEZA BALOZI WA JAPAN TANZANIA KWA JITIHADA ZA KUENDELEZA MICHEZO NCHINI.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Dokta Harrison G Mwakyembe amempongeza Balozi wa Japan nchini Tanzania Mheshimiwa Shinichi Goto kwa jitihada anazozionyesha kuendeleza uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Japan hususani katika sekta ya maendeleo ya michezo nchini.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Dokta Harrison G Mwakyembe akimpongeza Balozi wa Japan nchini Tanzania Mheshimiwa Shinichi Goto kwa jitihada anazozionyesha kuendeleza uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Japan hususani katika sekta ya maendeleo ya michezo nchini.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Dokta Harrison G Mwakyembe akimpongeza Balozi wa Japan nchini Tanzania Mheshimiwa Shinichi Goto kwa jitihada anazozionyesha kuendeleza uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Japan hususani katika sekta ya maendeleo ya michezo nchini.

Waziri Mwakyembe ameyasema hayo tarehe 21 Januari 2019, mbele ya viongozi wa vyama mbalimbali vya michezo nchini katika hafla maalumu iliyoandaliwa na Balozi wa Japan katika makazi yake yaliyopo ‘Kenyatta Drive 15’ ambapo amesema suala la jitihada zinazoendelea kwa moja ya miji ya Japan kuwa mwenyeji wa timu ya Tanzania itakayoshiriki mashindano ya Olimpiki 2020 Tokyo Japna, ni suala la upendo wa dhati na ushirikiano mzuri baina ya Tanzania na Japan kufanikisha maandalizi ya mashindano hayo.

IMG_3614“Mheshimiwa Balozi wa Japan nchini Tanzania kwanza kabisa nikushukuru sana kwa hafla hii uliyoiandaa ya kuweza kutuhalika viongozi mbalimbali wa michezo nchini, kiukweli ndani ya muda mfupi tu nimeona jitihada zako unazoziendeleza kutuhunganisha na watu wa Japan na moja ya miji nchini Japan kuwa mwenyeji wetu katika maandalizi ya mashindano ya Olimpiki 2020 Tokyo Japan, ni suala la upendo wa dhati kabisa na ushirikiano mzuri baina ya nchi hizi mbili kufanikisha maandalizi ya mashindano haya,” alisema Dokta Mwakyembe.

IMG_3508Aidha Dokta Mwakyembe ameipongeza Serikali ya Japan kwa masuala mbalimbali ambayo imefanya katika sekta ya michezo nchini kama vile kutengeneza uwanja mzuri wa Baseball uliopewa jina la “The Koshien” uliopo katika Shule ya Azania Sekondari jijini Dar es Salaam pamoja na kudhamini mashindano ya Riadha ya wanawake “Ladies First” yaliyofanyika kwa mafanikio makubwa kwa mara ya pili mfululizo.

IMG_3650“nichukue pia nafasi hii kuipongeza sana Serikali ya watu wa Japan kwa mambo mbalimbali ambayo imefanya katika sekta ya michezo nchini kama vile kututengenezea uwanja mzuri wa Baseball (The Koshien) uliojengwa katika shule ya Azania Sekondari pamoja na kudhamini mashindano ya “Ladies First” ambayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa na mafanikio makubwa katika kuibua vipaji vya wanariadha wanawake nchini,” alisema Mheshimiwa Mwakyembe.

Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Shinichi Goto akimuahidi Mheshimiwa Mwakyembe kuwa Serikali ya Japan itaendelea kuwa karibu na Tanzania katika masuala mbalimbali ya Maendeleo ikiwemo michezo kwa kutoa msaada pale inapoitajika
Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Shinichi Goto akimuahidi Mheshimiwa Mwakyembe kuwa Serikali ya Japan itaendelea kuwa karibu na Tanzania katika masuala mbalimbali ya Maendeleo ikiwemo michezo kwa kutoa msaada pale inapoitajika

Kwa upande wake Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Shinichi Goto amemuahidi Mheshimiwa Mwakyembe kuwa Serikali ya Japan itaendelea kuwa karibu na Tanzania katika masuala mbalimbali ya Maendeleo ikiwemo michezo kwa kutoa msaada pale inapoitajika ili kuhakikisha michezo mbalimbali nchini inapiga hatua na kupata timu zenye ushindani zaidi katika mashindano ya kimataifa.

250 total views, 2 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email5
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2019/01/21/mheshimiwa-mwakyembe-ampongeza-balozi-wa-japan-tanzania-kwa-jitihada-za-kuendeleza-michezo-nchini/">
RSS