NAGAI YAENDELEA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA TANZANIA KUELEKEA 2020 OLYMPIKI

Mwakilishi wa Kaimu Mtendaji Mkuu wa BMT na Afisa Maendeleo ya Michezo Neema Msitha akihoji jambo kwa ujumbe wa Mji wa Nagai hawapo pichani ulipotembelea Ofisi za BMT tarehe 22 Januari, 2019 kuimarisha ushirikiano wa nchi hizi mbili kabla ya 2020 Olympiki.
Mwakilishi wa Kaimu Mtendaji Mkuu wa BMT na Afisa Maendeleo ya Michezo Neema Msitha akihoji jambo kwa ujumbe wa Mji wa Nagai hawapo pichani ulipotembelea Ofisi za BMT tarehe 22 Januari, 2019 kuimarisha ushirikiano wa nchi hizi mbili kabla ya 2020 Olympiki.

Mji wa Nagai nchini Japan mwenyeji wa Tanzania wachezaji watakapoweka kambi  kabla ya kuelekea Tokyo Japan katika mashindano ya Olympiki 2020, wameendelea kuimarisha ushirikano ambapo Wawakilishi wamewasili nchini ili kusaini Mkataba wa ushirikiano huo pamoja na kukutana na baadhi ya Vyama washiriki wa michezo hiyo.

Ujumbe huo umewasili leo tarehe 22 Januari, 2019 katika Ofisi za chombo chenye mamlaka kisheria kusimamia michezo nchini Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kujadili mambo mbalimbali ya kushirikiana kabla ya kukutana na vyama na hatimaye tarehe 23 kukutana na Uongozi wa Wizara ili kusaini Mkataba wa kuimarisha ushirikiano wa Tanzania na Mji wa Nagai.

Mwenyeji wa ujumbe huo na Mwakilishi wa Kaimu Mtendaji Mkuu wa BMT Neema Msitha ameupokea na kufanya mazungumzo nao pamoja na kuhoji mambo mbalimbali ambayo Nagai itashirikiana na vyama shiriki vya mashindano hayo kabla na wakati watakapokuwa kambini nchini humo kabla ya kuelekea nchini Tokyo tayari kwa mashindano.

Mjumbe kutoka Mji wa Nagai Shin Saito (kulia) akifafanua jambo kwa Mwakilishi wa Mtendaji wa BMT baada ya kuuliza mambo watakayoshirikiana na Tanzania kabla na wakati wa kambi Mjini Nagai kuelekea Olympiki.
Mjumbe kutoka Mji wa Nagai Shin Saito (kulia) akifafanua jambo kwa Mwakilishi wa Mtendaji wa BMT Neema Msitha  baada ya kuuliza mambo watakayoshirikiana na Tanzania kabla na wakati wa kambi Mjini Nagai kuelekea Olympiki.

“Mnaweza kutupa ufafanuzi kidogo ni katika mambo gani Mji wa Nagai utaweza kuisaidia nchi yetu kabla na wakati wakiwa Mjini hapo kabla ya kuelekea rasmi katika mashindano nchini Tokyo,”aliuliza Neema.

Aidha, akifafanua hilo Mwakilishi kutoka Nagai Masaki Suzuki alisema kuwa, hawawezi kusema kitu husika watakachosaidia ila mawasiliano yakifanyika mapema katika suala lolote Uongozi wa  Mji wa Nagai utaangalia namna bora ya kushirikiana na Tanzania katika suala hilo.

Katibu Mkuu wa Kamati ya Michezo ya Watu wenye Ulemavu Tanzania (TPC) Tuma Dandi aliyekaa kwenye baiskeli ya watu wenye ulemavu kushoto akieleza baadhi ya changamoto ya wachezaji wa kundi hilo kufikia vigezo vya Oliympiki na kueleza kuwa wanahitaji usaidizi kidogo kufikia 2020 Oliympiki.
Katibu Mkuu wa Kamati ya Michezo ya Watu wenye Ulemavu Tanzania (TPC) Tuma Dandi aliyekaa kwenye baiskeli ya watu wenye ulemavu kushoto akieleza baadhi ya changamoto ya wachezaji wa kundi hilo kufikia vigezo vya Oliympiki na kueleza kuwa wanahitaji usaidizi kidogo kufikia 2020 Oliympiki kwa ujumbe huo.

Katika hatua nyingine Ujumbe huo baada ya kufanya mazungumzo na Baraza wameweza kukutana pia na Katibu wa Kamati ya Watu wenye Ulemavu Tanzania (TPC) Tuma Dandi ambaye naye alieleza baadhi ya mambo yanayowakabili wachezaji wa michezo mbalimbali ya kundi hilo na kuwaomba Wawakilishi hao wa Mji mwenyeji wa Tanzania kuona jinsi ya kusaidiana nao kufikia vigezo vya Olympiki na pia kupatiwa vifaa vya michezo yao.

Hata hivyo katika suala hilo Ujumbe huo ulieleza kulifikisha kwa Viongozi wa juu na mawasiliano zaidi yatafanyika kuona hilo linafanikiwa.

 

 

 

 

 

3,230 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email4
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2019/01/22/nagai-yaendelea-kuimarisha-ushirikiano-na-tanzania-kuelekea-2020-olympiki/">
RSS