KURUGENZI ZA MICHEZO BARA NA VISIWANI ZAKUTANA KUPANGA MIKAKATI YA PAMOJA KUBORESHA MICHEZO NCHINI.

Kurugenzi ya maendeleo ya Michezo Tanzania Bara na visiwani zimekutana katika kikao maalum kilichofanyika katika ofisi ya mkurugenzi wa maendeleo ya michezo uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Yusuph Omar Singo kwa lengo la kupanga mikakati ya pamoja kuboresha michezo nchini.

Viongozi wa Michezo Tanzania Bara na Visiwani wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kikao cha kupanga mikakati ya pamoja kuboresha michezo nchini.
Viongozi wa Michezo Tanzania Bara na Visiwani wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kikao cha kupanga mikakati ya pamoja kuboresha michezo nchini.

Akizungumza katika kikao hicho leo tarehe 13 Februari, 2019, Mkurugenzi Singo amesema ni wakati sasa wa kuhakikisha michezo nchini inapiga hatua zaidi zikiwemo timu za Tanzania Bara na visiwani kufanya vizuri katika mashindano ya kitaifa na kimataifa hivyo wapo katika upangaji wa mikakati ya pamoja kuhakikisha michezo inaboreshwa nchini.

IMG_3994“Lengo la sisi kukaa katika kikao hiki na ndugu zetu wa visiwani ni kuhakikisha michezo nchini inapiga hatua zaidi zikiwemo timu zetu kufanya vizuri katika mashindano ya kitaifa na kimataifa, hivyo tumeona ni vyema tukaweka mikakati ya pamoja ili kuhakikisha tunaboresha michezo yetu nchini,”alisema Singo.

Aidha Mkurugenzi Singo amesema wamepanga kuwa na vikao vya pamoja vya mara kwa mara na kutoa mrejesho kwa viongozi wa juu kuhusu masuala ambayo yatakuwa yanajadiliwa katika vikao hivyo sanjari na kuvikutanisha vyama pacha ili kuvijengea utamaduni wa kuwa na sura ya kitaifa.

IMG_4001“tumepanga kuwa na vikao vya pamoja vya mara kwa mara na kutoa mrejesho wa masuala yatakayokuwa yanajadiliwa katika vikao hivyo kwa viongozi wetu wa juu lakini pia tunapanga kuvikutanisha vyama vyetu pacha ili kuvijengea utamaduni wa kuwa na sura ya kitaifa,”alisema Singo.

344 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email5
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2019/02/13/kurugenzi-za-michezo-bara-na-visiwani-zakutana-kupanga-mikakati-ya-pamoja-kuboresha-michezo-nchini/">
RSS