NKENYENGE AWATAKA MAAFISA MICHEZO KUWAJIBIKA IPASAVYO ILI MICHEZO IONEKANE THAMANI YAKE.

Kaimu Katibu Mkuu wa BMT akieleza jambo kwa viongozi wa vyama vya michezo shiriki katika mchezo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki hawapo pichani wakati wa kikao nao kupanga namna ya kushiriki michezo hiyo Agosti mwaka huu nchini Burundi.
Kaimu Katibu Mkuu wa BMT akieleza jambo kwa Maafisa Michezo wa Mkoa wa Dar es salaam alipokaa nao kupanga mikakati ya kuanzisha vyanzo vya mapato vya sekta ya michezo nchini, kikao kilichokaliwa Februari 15, 2019 Jijini Dar es salaam.

Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Alex Nkenyenge amewataka Maafisa Michezo nchini kuacha kulalamika badala yake wawajibike ipasavyo ili thamani yao na michezo kwa ujumla iweze kuonekana.

Rai hiyo ameitoa Februari 15, 2019 wakati Baraza lilipoandaa kikao na Maafisa Michezo wa Mkoa wa Dar es salaam na kwa niaba ya waliopo Mikoa mingine kwa lengo la kujadili namna bora kukusanya mapato kupitia vyanzo mbalimbali vya mapato  kupitia michezo ili michezo iweze kujiendesha yenyewe kupitia vyanzo vyake.

“Tunavyo vyanzo vingi vya mapato ambavyo vinaweza saidia maendeleo ya michezo, kwahiyo ni wajibu wetu tukae tuvijadili na kuviandikia ili viingie kwenye Sheria na kanuni za Michezo ili tuweze kukusanya mapato yatakayowezesha maendeleo ya michezo na tuache kulalamika badala yake tuwajibike,”alisema Nkenyenge na kuongeza kuwa:

”Thamani yako itaonekana pale tu mchango wako utakapoonekana, tunatakiwa tutekeleze mifumo pamoja na siasa, yaani tunatakiwa kuitekeleza ilani ya chama vilivyo kwakuwa haikuacha michezo, tunatakiwa kuwatambua Wajumbe wa Kamati zetu na kuhakikisha zinafanya kazi, shule zinazofundisha michezo katika halmashauri zetu na Mikoa,”alieleza Nkenyenge.

Nkenyenge aliwaeleza Maafisa Michezo hao wa Dar es salaam pamoja na Mikoa mingine kuwa, wahakikishe wanaandaa vikao na Wajumbe wa Kamati zao zikiwemo za Mikoa na Wilaya mapema mwaka huu wa fedha na kumshirikisha, lakini pia wawe na takwimu za vyama vya michezo, gym za michezo zilizomo katika maeneo yao, shule za michezo,  kuwajuwa wanamichezo pamoja na kuisoma vyema Sheria ya BMT.

Kwa upande wake Afisa Michezo wa Mkoa wa Dar es salaam Adolph Halii alieleza kuwa, Sheria ya BMT ina nguvu sana na yapo mengi ambayo hatujayafanyia kazi, lakini anakubaliana na Mtendaji wa BMT kuwa lazima Maafisa Michezo kukaa pamoja na kubuni vyanzo thabiti vya mapato kupitia kwenye michezo ili michezo iweze kujiendesha kwa kutumia vyanzo vyake.

Halii aliendelee kuwa, michezo inafaida nyingi kwa jamii ikiwemo kujenga afya, kuleta ajira na kuleta mahusiano mazuri kwa jamii na wanafunzi wengi wanalipenda somo la michezo na linawabeba katika ufaulu, huku akiomba Serikali kuona umuhimu wa somo la PE kuingia katika hesabu za ufaulu wa mitihani ya mwisho pamoja na kuingia kama somo katika michepuo.

Aidha, katika kikao hicho, Maafisa Michezo hao wameshauri Serikali kuona umuhimu wa kuwaweka Wakurugenzi kuwa ndiyo Wenyeviti wa Kamati za Michezo badala ya Makatibu Tawala kwakuwa wao ndio wenye fundi la pesa ambapo watazisikiliza changamoto za michezo moja kwa moja wawapo kwenye vikao vya Kamati hizo na kuisaidia michezo.

IMG_20190215_115840_3Maafisa Michezo wa Mkoa wa Dar es salaam wakiwa katika kikao kujadili vyanzo vya mapato ya michezo.

 

Kikao hicho kiliwahusisha Maafisa BMT akiwemo Mtendaji wa BMT Alex Nkenyenge, Mwenyekiti wa Kikao na Afisa Maendeleo ya Michezo, Milinde Mahona, Afisa Mipango George Msonde, Mhasibu Alinanuswe Mwamundela, Afisa Michezo Mkoa Dar es salaam Adolph Halii, Maafisa Michezo Manispaa ya Temeke Ingridy Kimario, Ilala Salim Sanga, Kinondoni Respis Bilehe na Ubungo Fredrick Kadewele.

Maafisa wa BMT wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Michezo wa Mkoa wa Dar es salaam mara baada ya kikao cha kujadili vyanzo vya mapato ya michezo kilichofanyika Februari 15 jijini Dar es salaam.
Maafisa wa BMT wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Michezo wa Mkoa wa Dar es salaam mara baada ya kikao cha kujadili vyanzo vya mapato ya michezo kilichofanyika Februari 15 jijini Dar es salaam.

464 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email4
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2019/02/15/nkenyenge-awataka-maafisa-michezo-kuwajibika-ipasavyo-ili-michezo-ionekane-thamani-yake/">
RSS