NKENYENGE AWATAKA VIONGOZI KUWASIMAMIA WACHEZAJI IPASAVYO WARUDI NA USHINDI

Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Alex Makoye Nkenyenge amewataka Viongozi wanaokwenda na timu ya watu wenye ulemavu wa akili nchini Abu dhabi katika mashindano ya dunia ya michezo ya kundi hilo kuhakikisha wanawasimamia kwa umakini wachezaji wetu ili waiwakilishe nchi vyema kwa kurudi na ushindi.

IMG_4867Hilo amelisema leo tarehe 08 Machi, 2019 wakati alipokuwa akiikabidhi bendera timu hiyo ya Watu wenye Ulemavu wa akili wanaokwenda kwenye mashindano ya dunia yanayotarajiwa kufanyika nchini Abu dhabi kuanzia tarehe 12 hadi 22 kwa kushirikisha nchi 200.

“Viongozi hakikisheni mnawasimamia vyema vijana wetu ili waweze kufanya vizuri na kuiwakilisha nchi kwa ushindi,”alisema Nkenyenge.

Aidha, Nkenyenge amekitaka Chama kinachohusika na kundi hilo kusimamia fursa za kundi hilo vyema ili kuwapata vijana watakaoiwakilisha nchi vizuri katika mashindano mbalimbali kwa kuiletea sifa nchi yetu.

Aliendelea kuwa, Serikali imeweka utaratibu timu yoyote inapotaka kwenda kwenye mashindano, viongozi wa chama husika kuhakikisha wanapeleka wachezaji wenye vigezo watakaoiwakilisha nchi kwa ushindi badala ya kupeleka wachezaji wengi ambao hawana vigezo vya kuiletea nchi sifa mbaya ya kukosa ushindi.

Lakini pia amewashauri viongozi wa chama hicho kupeleka timu kambini katika Mikoa ambayo inaendana na hali ya nchi ambako mashindano yanafanyika ni vizuri zaidi ingawa Waafrika huwa wanaweza kucheza katika hali yoyote bila tatizo.

Kwa upande wake Kocha na Mwakilishi kutoka Baraza la Michezo la Zanzibar (BMTZ) Saada Hamad Ali alisema kuwa, wachezaji wao wako tayari kwa ushindani na wamejiandaa vizuri na hawajawahi kurudi bila ushindi watanzania watoe hofu.

“Msituangalie ulemavu wetu angalieni uwezo wetu, lakini pia tunaomba Wizara pamoja na Mabaraza ya Michezo Tanzania gusweni na uwakilishi wa watoto hawa, huwa wanafanya vizuri kila tunapoenda katika mashindano,”alieleza Saada.

Katika hatua nyingine Mratibu Mkuu wa shughuli za Zanzibar hapa Tanzania Bara Issa Mlingoti amewashukuru wafadhili waliowezesha kambi ya vijana hao Arusha na kuwataka wachezaji hao kufanya vizuri kwa kufuata nyayo za Serengeti Boys.

Timu ya Watu wenye ulemavu wa akili (Special Oliympic) inayoshiriki mashindano ya dunia nchini Abu dhabi inawakilishwa na wachezaji 15 wanawake 7 na wanaume 8 katika michezo miwili ikiwemo wa Wavu na Riadha.

65 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email4
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2019/03/08/nkenyenge-awataka-viongozi-kuwasimamia-wachezaji-ipasavyo-warudi-na-ushindi/">
RSS