VYAMA VYA MICHEZO VYATAKIWA KUJIPIMA KULINGANA NA MASHINDANO YAO KIMATAIFA SIYO NYUMBANI

Kaimu Katibu Mtendaji wa BMT Makoye Alex Nkenyenge (katikati) akiongea na Viongozi wa Vyama vya Michezo ukumbi wa Utaifa kuhusu maandalizi ya "All African Game" Machi, 19, kulia ni Rais wa TOC Gulam Rashid na kulia ni Afisa Michezo BMT Neema Msitha.
Kaimu Katibu Mtendaji wa BMT Makoye Alex Nkenyenge (katikati) akiongea na Viongozi wa Vyama vya Michezo ukumbi wa Utaifa kuhusu maandalizi ya “All African Game” Machi, 19, kushoto ni Rais wa TOC Gulam Rashid na kulia ni Afisa Michezo BMT Neema Msitha.

 

Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Makoye Alex Nkenyenge amewataka Viongozi wa Vyama vya Michezo kupima viwango vya wachezaji wao kulingana na kushiriki mashindano ya Kimataifa na siyo kujipima kwa kushiriki mashindano ya hapa nchini.

Hayo ameyasema tarehe 19 Machi, 2019 alipowaita viongozi wa vyama vya michezo na kufanya mazungumzo nao kuhusu viwango vya wachezaji wao Kimataifa pamoja na kufanya maandalizi ya michezo shiriki katika michezo ya Jumuiya ya nchi za Afrika (All African Game).

“Vyama vya Michezo pimeni viwango vya wanamichezo wenu kulingana mashindano ya Kimataifa na siyo kujipima kwa mashindano ya hapa nchini,”alieleza Nkenyenge.

 

IMG_5250IMG_5251         Kikao kikiendelea kati ya Mtendaji Mkuu BMT na Viongozi wa baadhi ya Vyama vya Michezo

BMT liliviandikia barua vyama vyote kushiriki katika kikao hicho hata kama hawashiriki michezo hiyo ili kujadiliana nao mambo mengi yanayohusu maendeleo ya michezo nchini ikiwemo kila Viongozi vya vyama kuangalia fursa za wanamichezo wao kushiriki mashindano mbalimbali ya Kimataifa ili kuwa na viwango hivyo kwakuwa kila mchezo una mashindano yake ya Afrika na Dunia lakini pia kuondoa majungu kila chama kijue kilichoongelewaz .

Nkenyenge alieleza kuwa, lengo kuu la kikao hicho ni kuwapa mrejesho wa kikao alichoriki mwanzoni mwa mwezi huu nchini Morocco ambapo michezo hiyo itafanyika mwaka huu kuanzia mwezi Agosti hadi Septemba ili maandalizi yaweze kufanyika kwa michezo itakayoshiriki ili iweze kuiwakilisha nchi kwa ushindi.

“Timu zitakazokidhi vigezo vya kwenda lazima zikashindane na siyo kwenda kutembea,”alisisitiza Nkenyenge.

Kwa upande wake Rais wa Kamati ya Olympiki Tanzania (TOC) Gulam Rashid alisema kuwa, kila kiongozi anataka mchezo wake ushiriki lakini lazima tuanze kuweka sawa maandalizi kabla ya kwenda kwenye mashindano.

Michezo iliyopendekezwa kushiriki katika mashindano hayo ambayo imo katika michezo hiyo na ina vigezo vya ushiriki ni Riadha, Gofu ya Wanawake, Judo na Soka la Wanawake ingawa wameelekezwa kuendelea kujifua na mazoezi ya kutosha ili ziiwakilishe nchi vizuri.

 

120 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email4
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2019/03/19/vyama-vya-michezo-vyatakiwa-kujipima-kulingana-na-mashindano-yao-kimataifa-siyo-nyumbani/">
RSS