HATIMAYE NGUMI ZA KULIPWA ZAPATA VIONGOZI WA KUONGOZA KATIKA CHOMBO KIMOJA

Viongozi wa Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanmzania (TPBRC) waliochaguliwa tarehe 31 Machi, 2019
Viongozi wa Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanmzania (TPBRC) waliochaguliwa tarehe 31 Machi, 2019 wakimsikiliza Kaimu Katibu Mtendaji wa BMT Alex Nkenyenge hayupo pichani akiwaeleza jambo baada ya kuapishwa.

 

Mchezo wa ngumi za kulipwa nchini umefanikiwa kwa mara ya kwanza kuwa katika chombo kimoja kijulikanacho kama Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBRC) cha kuusimamia na hatimaye viongozi wa kuongoza chombo hicho wamepatikana katika uchaguzi uliofanyika jana tarehe 31 Machi, 2019 katika ukumbi wa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Viongozi waliopatika katika uchaguzi huo ni Rais ambapo nafasi hiyo imeenda kwa Joe Joseph Annea aliyeibuka na kura 108 kati ya kura 120 halali dhidi ya mpinzani wake Ally Bakari Champion aliyeambulia kura 12, wakati nafasi ya Makamu wa Rais imechukuliwa na Agapita Basily kwa kura 35 huku mpinzani wake Chaurembo Palasa aliyejishindia kura 31 na kura 54 hazikupigwa kabisa, nafasi ya Katibu Mkuu amenyakuliwa na Yahya Salum Poli kwa kura 101 dhidi ya mpinzani wake Chatta Michael aliyeambulia kura 17 huku kura 2 zikiharibika.

Nyingine ni nafasi za wajumbe ambapo kwa mujibu wa Katiba ya TPBRC wanatakiwa wajumbe wanne waliopata kura nyingi zaidi nao ni Japhet Joseph Kaseba kura 103, Bakari Songolo kura 89, Hamis Kimanga kura 85 na Nassoro Chuma mwenye kura 76.

Aidha, Mwenyekiti wa Uchaguzi Benson Chacha Afisa Michezo wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) baada ya kutangaza matokeo ya uchaguzi aliwaeleza Viongozi waliochaguliwa kuwa nafasi ya Mweka hazina haikupata mgombea hivyo ndani ya muda mfupi wa uongozi wao wahakikishe wanaitisha uchaguzi mdogo kujaza nafasi hiyo.

Katika hatua nyingine Kaimu Katibu Mtendaji wa BMT Makoye Alex Nkenyenge kwa niaba ya Waziri mwenye dhamana ya Michezo Mhe. Mwakyembe ameipongeza Kamati ya muda ya ngumi za kulipwa pamoja wadau wa mchezo huo kufanikisha zoezi hilo la uchaguzi na ngumi za kulipwa kuongozwa na chombo kimoja.

Kaimu Katibu Mtendaji wa BMT Alex Nkenyenge akieleza jambo kwa wapiga kura kabla ya uchaguzi tarehe 31 Machi wakati wa uchaguzi wa viongozi waTPBRC
Kaimu Katibu Mtendaji wa BMT Alex Nkenyenge akieleza jambo kwa wapiga kura kabla ya uchaguzi tarehe 31 Machi wakati wa uchaguzi wa viongozi waTPBRC

Nkenyenge amewataka Viongozi hao kufanya kazi kwa mujibu wa katiba ya TPBRC na kwa kufuata Sheria ya Baraza la Michezo la Taifa pamoja na kuhakikisha kila mdau ananufaika kulingana na jasho lake na waepuke kumwonea mtu yeyote.

Kwa upande wake Rais wa Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania(TPBRC) Joe Joseph Annea amewashukuru wapiga kura wake na kuwataka waendelee kuonyesha umoja waliowaonyesha wakati wakiwa katika kamati ya muda lakini pia waachana na makundi na anawaahidi Uongozi wake utatenda haki kwa kila mdau na ngumi za kulipwa zitaendelea zaidi na kuliletea sifa Taifa.

 

Baadhi ya Wapiga kura wa ngumi za kulipwa wakifuatilia utaratibu kabla ya uchaguzi kuanza
                       Baadhi ya Wapiga kura wa ngumi za kulipwa wakisubiri muda wa kupiga kura

 

553 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email4
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2019/04/01/hatimaye-ngumi-za-kulipwa-zapata-viongozi-wa-kuongoza-katika-chombo-kimoja/">
RSS