BASEBALL NA SOFTBALL WATAKIWA KUITENDEA HAKI BENDERA YA TANZANIA

Kaimu Katibu Mtendaji wa BMT Mkoye Alex Nkenyenge akikabidhi bendera kwa Nahodha wa Timu ya mchezo wa Baseball na Softball Ally Abdallah wakielekea Nchini Kenya tarehe 3 Aprili katika mashindano ya kupata viwango vya Olympiki yanayotarajiwa kufanyika tarehe 5 hadi 7 nchini Nairobi Kenya.
Kaimu Katibu Mtendaji wa BMT Mkoye Alex Nkenyenge akikabidhi bendera kwa Nahodha wa Timu ya mchezo wa Baseball na Softball Ally Abdallah wakielekea Nchini Kenya tarehe 3 Aprili katika mashindano ya kupata viwango vya Olympiki yanayotarajiwa kufanyika tarehe 5 hadi 7 nchini Nairobi Kenya.

Wachezaji wa timu ya ‘Baseball na softball’ watakiwa kuitendea haki  bendera ya Tanzania  kwa kuipeperusha kwa kufanya vizuri katika mashindano wanayoshiriki nchini Kenya ya kutafuta viwango kwa timu za Afrika yanayotarajiwa kuanza tarehe 5 na kuhitimishwa  tarehe  7 Aprili, 2019.

Rai hiyo ameitoa Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT)    Makoye Alex Nkenyenge baada ya kukabidhi bendera kwa timu hiyo ya Taifa ya Mchezo huo iliyowakilishwa na wachezaji 14 na Viongozi 6 wanaotarajia kuondoka tarehe 3 alfajiri kuelekea katika mashindano hayo nchini Kenya.

“Hakikisheni mnaitendea haki bendera ya nchi kwa kufanya vizuri katika mashindano hayo,”alisema Nkenyenge.

Aliendelea kwa kuwataka Wazazi, Walimu na Wakuu wa Taasisi zinazoendeleza vijana kuwapa fursa  za kushiriki katika  michezo kwani inaweza kuwapeleka katika hatua nzuri kama fani zingine kama kuwapatia ajira, kuwajenga kiafya na mengineyo, lakini pia amewataka vijana hao kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania ikiwemo Visiwani na Bara kuhakikisha wanashirikiana ili kufanya vyema zaidi.

“Kuna wazazi ambao hawataki watoto wao washiriki katika michezo wakiamini kuwa wanapoteza muda kitu ambacho siyo sahihi lakini timu ikifanya vizuri wanashangilia, Wazazi, Waalimu na Taasisi zinazoendeleza vijana wapeni fursa Vijana ya kucheza,”alisisitiza Nkenyenge.

Hata hivyo Nkenyenge amewahakikishia kuwa Baraza liko pamoja nao na Watanzania kwa ujumla kwa dua na maombi ya hali zote kuona kuwa wanafanya vyema, huku akiwapa moyo kuwa nchi wanazoshindana nazo ikiwemo mwenyeji Kenya na Uganda ni timu changa kushinda Tanzania.

Kwa upande wake Nahodha wa timu hiyo Ali Mohamedi Abdallah amewaomba Watanzania waendelee kuwaombea dua  lakini pia amewahakikishia kurudi na ushindi kwakuwa wamejiandaa vya kutosha na Mwalimu wao Hirok ana viwango na amewaandaa vya kutosha.

Katika hatua nyingine Katibu wa Chama cha mchezo wa Baseball na Softball (TaBSA) Alpherio Nchimbi ameeleza kuwa timu za Afrika wamejiandalia mazingira mazuri ya kufuzu viwango vya kimataifa kwa kuandaa mashindano mbalimbali kwa mwaka huu.

 

252 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email4
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2019/04/02/baseball-na-softball-watakiwa-kuitendea-haki-bendera-ya-tanzania/">
RSS