SERIKALI YAPOKEA UGENI KUTOKA AFRIKA YA KUSINI KUWEKA USHIRIKIANO KATIKA KUWAINUA VIJANA

Kaimu Katibu Mtendaji wa BMT mwenye suti katikati akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe kutoka Afrika ya Kusini kabla mazungumzo nao kuhusu ushirikiano katika kuwainua Vijana.
Kaimu Katibu Mtendaji wa BMT mwenye suti katikati akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe kutoka Afrika ya Kusini kabla mazungumzo nao kuhusu ushirikiano katika kuwainua Vijana, kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya maendeleo ya Vijana (NYDA) Ankie Motsoah.

Serikali imepokea Ujumbe kutoka Serikali ya Afrika ya Kusini kupitia Taasisi yake ya maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Rais ya nchi hiyo ijulikanayo kama (National Youth development agency) ambayo ni Taasisi ya Serikali yenye lengo la kuwajenga vijana katika nyaja tofauti, wamekuja nchini kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu kutaka ushirikiano na Tanzania katika kuwainua Vijana kupitia sekta tofauti ikiwemo Michezo kwa kujenga ushirikiano, kujitambua pamoja na kujiamini katika kujiletea maendeleo.

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) leo tarehe 2 Aprili, 2019 limefanya mazungumzo na Ujumbe huo katika kuwainua Vijana wa Tanzania kupitia Sekta ya Michezo katika kujiamini, kujitambua, ushirikiano na kuwajenga katika umoja wa Kitaifa, na katika sekta ya michezo wamekubaliana kushirikiana katika maeneo matatu (3).

Uanzishwaji wa kambi za michezo, hili ni moja ya suala ambalo wamefanya majadiliano ya kuwa linaweza kuwajenga vyema vijana ambapo wakiwa kambini wanaweza kufundishwa mambo mbalimbali ikiwemo Utawala, Mazingira, Afya, Ujasiriamali na mambo mengi mazuri ya kuwajenga Vijana katika maisha yao.

 

Kikao cha mazungumzo ya masuala ya ushirikiano sekta ya michezo kati ya BMT na Taasisi ya Maendeleo ya Vijana Afrika ya Kusini (NYDA) Aprili 2, 2019 Uwanja wa Uhuru.
Kikao cha mazungumzo ya masuala ya ushirikiano sekta ya michezo kati ya BMT na Taasisi ya Maendeleo ya Vijana Afrika ya Kusini (NYDA) Aprili 2, 2019 Uwanja wa Uhuru.

Kuhamasisha maendeleo ya michezo ya jadi ambayo ilionekana baada ya kutawaliwa na wakoloni michezo ya jadi ya Kiafrika imeonekana kutupiliwa mbali na kuiga michezo mbalimbali iliyoletwa na wakoloni. Hivyo BMT imependekeza ushirikiano katika sehemu ya michezo ya jadi kutawafanya vijana kuutambua utamaduni wetu wa Afrika badala ya kuiga tamaduni za nje na kusahau za kwetu.

Aidha, mapendekezo ya BMT ya ushirikiano katika sekta ya Michezo vilevile wamependekeza washirikiane katika Elimu kwa Michezo (Physical Education) kuona namna ya kuwaandaa vijana darasani na uwanjani kuhusu sheria, kanuni na taratibu mbalimbali za michezo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Taasisi hiyo ya maendeleo ya Vijana nchini Afrika ya Kusini (NYDA) Ankie Motsoah amesema kuwa, Serikali na Viongozi wake wamedhamiria kushirikiana na Tanzania katika sekta ya tofauti katika kuwainua vijana, na wanaendelea na mazungumzo na taasisi zingine waliodhamiria kushirikiana nazo na watakapokamilisha mazungumzo watasaini makubaliano hayo.

 

 

104 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email4
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2019/04/02/serikali-yapokea-ugeni-kutoka-afrika-ya-kusini-kuweka-ushirikiano-katika-kuwainua-vijana/">
RSS