KATIBU MKUU WA WIZARA YENYE DHAMANA YA MICHEZO BI SUSAN MLAWI APOKEA SHAIRI MAALUM KWA AJILI YA TAIFA STARS

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Susan Mlawi amepokea Shairi Maalum lililotungwa kwa ajili ya Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kutoka kwa mshairi na mwanasheria kitaaluma Bi. Aisha Kingu.

IMG_6378

Akipokea Shairi hilo leo tarehe 8 April 2019, katika ukumbi wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Bi. Susan amesema ni uzalendo mkubwa ulioonyeshwa na Bi. Aisha kwani Taifa kwa sasa linafanya vizuri katika michezo mbalimbali ukiwepo mchezo wa mpira wa miguu, ambapo timu ya Taifa imefuzu kucheza michuano ya Afcon 2019 itakayofanyika nchini Misri mwezi Juni mwaka huu.

IMG_6392

“kwa kweli kwanza kabisa nimpongeze sana Bi. Aisha kwa kuonyesha uzalendo wa hali ya juu sana kuandaa shairi kwa Timu yetu ya Taifa ambayo imetutoa kimasomaso kwa kutupeleka katika michuano ya Afcon 2019 nchini Misri, kwani Taifa kwa sasa linafanya vizuri katika michezo mbalimbali,”alisema Bi. Susan.IMG_6404

Aidha kwa upande wake Bi. Aisha amesema kitu kikubwa kilichomsukuma kuandika Shairi hilo kwanza kabisa ni ushindi ulioletwa na Taifa stars, Ari iliyoonyeshwa na mashabiki wa Tanzania kwa kuungana pamoja kwa amani kulishangilia Taifa wakati wa kutafuta tiketi ya kufuzu kombe la mataifa Barani Afrika.

126 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email4
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2019/04/08/katibu-mkuu-wa-wizara-yenye-dhamana-ya-michezo-bi-susan-mlawi-apokea-shairi-maalum-kwa-ajili-ya-taifa-stars/">
RSS