BMT LAONGEZA MIEZI MIWILI KWA VYAMA VYA MICHEZO KUTIMIZA MAAGIZO YAKE

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limeviongezea Vyama vya Michezo miezi miwili kuhakikisha vinatimiza maelekezo lililotoa Octoba 10, 2018 lilipokutana na Viongozi wake na kutoa Mwongozo ambao utekelezaji wake ulikuwa ndani ya kipindi cha miezi sita (6) hadi tarehe 31 Machi, 2019. Lakini limeongeza muda huo hadi kufikia Mei 31, 2019.

IMG_6775Maelekezo hayo kwa Vyama vya Michezo ameyatoa Kaimu Katibu Mtendaji Makoye Alex Nkenyenge Aprili 9, 2019 wakati alipofanya mkutano na vyombo vya habari ili kuhakikisha ujumbe huo unawafikia walengwa kwa wakati.

“Bodi ya BMT imeamua iviongezea muda wa miezi miwili Vyama vya Michezo kutekeleza maagizo tuliyotoa Octoba 10, 2019 hadi kufikia Mei 31, 2019,”alisema Nkenyenge.

Nkenyenge ameeleza kuwa,  Bodi ya Baraza imepitia utekelezaji wa agizo lile na kugundua kuwa Vyama na Mashirikisho yetu yameshindwa  kufikia matarajio na hivyo, kuamua kuongeza kipindi cha miezi miwili (2) hadi kufikia Mei 31, 2019 ambapo Chama/Shirikisho linatakiwa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji kwa barua ikionesha,  Anwani ya Ofisi ya Chama/Shirikisho (Mtaa/Namba ya Nyumba; pamoja na Akaunti ya Chama husika;

Mengine ni Mpango kazi (Action Plan) na sio Kalenda ya Matukio ikionesha shughuli iliyopangwa, matokeo tarajiwa, muda wa utekelezaji na gharama zitakazotumika.

Lakini pia, taarifa ya Mendeleo ya Chama ikionesha, Programu kwa Vijana, Walimu, Waamuzi Kitaifa; Mashindano ya Kitaifa yaliyofanyika kuanzia mwaka (2016 – 2019); Ushiriki katika Mashindano ya Kimataifa na Matokeo yake pamoja na kuleta taarifa za ulipaji wa Ada kwa kipindi cha kuanzia 2016 – 2019.

Aidha, Nkenyenge alitoa taarifa kwa  Vyama na Mashirikisho yenye hadhi ya Kitaifa na wale walio na Msamaha wa Msajili kuwa, kushindwa kutekeleza maagizo hayo ni kukiuka Sheria ya Baraza la Michezo la Taifa.

“Napenda kutoa taarifa kwa Vyama na Mashirikisho yenye hadhi ya Kitaifa na wale walio na Msamaha wa Msajili kuwa, kushindwa kutekeleza maagizo hayo ni kukiuka Sheria ya Baraza la Michezo la Taifa,”alisisitiza Nkenyenge.

Alihitimisha kwa kusema kuwa, hadi kufikia tarehe 31 Mei, 2019 Chama ama Shirikisho litakaloshindwa kuwasilisha litashughulikiwa kwa mujibu wa Sheria ikiwemo kuwasilisha maombi kwa Mheshimiwa Waziri kuomba Chombo hicho kifutwe ili kupisha Wananchi wenye mapenzi na Mchezo husika kujipanga ili kuendeleza vipaji na kutoa ajira kupitia michezo badala ya kuendelea kulea uzembe wa Viongozi wasiojali Maendeleo ya Michezo na Taifa kwa ujumla.

Katika hatua nyingine, Nkenyenge kwa niaba ya Bodi ya BMT amewashukuru Wadau wa Michezo kwa ushirikiano na Vyama/Mashirikisho mbalimbali ya Michezo katika nyakati zote na kusema kuwa Baraza linaomba ushirikiano huu uendelee kwa mustakabali na Ustawi wa Michezo na Taifa letu.

 

 

 

 

1,853 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email5
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2019/04/09/bmt-laongeza-miezi-miwili-kwa-vyama-vya-michezo-kutimiza-maagizo-yake/">
RSS