WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFUNGUA AFCON U17 2019, TAIFA NA AZAM KUWAKA MOTO.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa, leo tarehe 14 April 2019, amefungua michuano ya kombe la mataifa Barani Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka kumi na saba (U17), itakayofanyika hapa nchini kwa siku kumi na nne katika viwanja vya Azam Complex na Taifa Jijini Dar es Salaam.

IMG_3505

Akifungua mashindano hayo uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kwa mechi ya wenyeji Tanzania dhidi ya Nigeria, Mhe. Majaliwa amesema licha ya kuwepo kwa viingilio katika michuano hiyo, serikali imeamua kwa mechi zote zinazofuata itakuwa ni bure hivyo ni vyema wananchi wakajitokeza kwa wingi kushuhudia mashindano hayo na kuishangilia timu ya vijana ya Serengeti Boys ambayo ipo kundi moja na Timu za Nigeria, Uganda pamoja na Angola.

IMG_3419

“Ndugu wanamichezo mliojitokeza leo kwanza kabisa niwapongeze sana kwa kuja leo katika ufunguzi huu, ambapo leo tumeweka historia katika serikali yetu ya awamu ya tano, kwa mashindano haya kufanyika hapa nchini kwetu, hivyo natamka rasmi kuwa mashindano haya yamefunguliwa, na kuanzia mechi zijazo kutakuwa hakuna viingilio, hivyo watanzania njooni tuishangilie timu yetu na kushuhudia kandanda safi linalochezwa na vijana wetu” alisema Mhe. Majaliwa.

IMG_3473

Mashindano ya Afcon U17 yanayoanza leo tarehe 14 April 2019, yatafikia tamati tarehe 28 April 2019, kwa mchezo wa Fainali kupigwa katika dimba la uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

4,397 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email5
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2019/04/14/waziri-mkuu-kassim-majaliwa-afungua-afcon-u17-2019-taifa-na-azam-kuwaka-moto/">
RSS