CAMEROON MABINGWA AFCON U17 2019

Timu ya Taifa ya Cameroon kwa vijana wenye umri chini ya miaka Kumi na Saba (U17) imefanikiwa kunyakuwa kombe la michuano ya mataifa Barani Afrika (AFCON U17), iliyokuwa inachezwa hapa nchini baada ya kuifunga timu ya Taifa ya Guinea kwa mikwaju ya penati (4-3) katika mchezo uliochezwa leo tarehe 28 April 2019, uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Cameroon imefanikiwa kuchukuwa ubingwa huo baada ya kuwa na muendelezo mzuri tangu kuanza kwa michuano hiyo tarehe 14 April 2019, baada ya kufanikiwa kumaliza kinara katika kundi B lililojumuisha timu za Morocco, Guinea pamoja na Senegal.

Aidha timu za Nigeria, Angola, Cameroon pamoja na Guinea zimefanikiwa kufuzu kucheza katika michuano ya kombe la Dunia kwa vijana wenye umri chini ya miaka kumi na saba (U17) itakayofanyika nchini Brazil mwaka 2020.

10 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email5
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2019/04/28/cameroon-mabingwa-afcon-u17-2019/">
RSS