HARAKATI ZA KUUSAMBAZA MCHEZO WA WOODBALL NCHINI ZAENDELEA

Katika harakati za kuusambaza mchezo wa woodball nchini Tanzania, klabu ya umoja chini ya mwalimu Nicholaus Achimpota imeendesha mafunzo ya siku moja kwa baadhi ya maafisa wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na waandishi wa Habari nchini.

Akizungumza na vyombo vya Habari leo tarehe 9 Mei 2019, mwalimu Achimpota amesema lengo la kutoa mafunzo hayo ni kuhakikisha kuwa wananchi kupitia waandishi wa Habari wanaufahamu mchezo huo jinsi ya kuucheza na sheria zake.

“ndugu waandishi wa habari lengo kubwa hasa la kuendesha mafunzo haya kwenu ni kuhakikisha kuwa wananchi kupitia nyinyi wanaufahamu mchezo huu jinsi unavyochezwa na sheria zinazotumika katika mchezo,”alisema Mwalimu Achimpota.

Aidha Mwalimu Achimpota amesema mchezo huo unaweza kuchezwa na watoto mpaka watu wazima wenye umri wa miaka 90 mpaka 100, na lengo lingine ni kupunguza suala la utoro shuleni kwani ni mchezo unaochezwa na watu wote wa kike kwa kiume.

“mchezo huu unaweza kuchezwa na watoto mpaka watu wazima wenye umri wa miaka 90 mpaka 100, lakini pia tumelenga kupunguza suala utoro shuleni baada ya kuutambulisha mchezo huu mashuleni kwani ni mchezo ambao unachezwa na watu wote wa kike na kiume,”alisema Mwalimu Achimpota.

 

 

3,307 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email5
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2019/05/09/harakati-za-kuusambaza-mchezo-wa-woodball-nchini-zaendelea/">
RSS