TENGA ATETA NA VIONGOZI WA TOC KUHUSU KUIMARISHA MICHEZO NCHINI

Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa Leodeger Tenga akiweka kumbukumbu ya yale ayasemayo Kaimu Mtendaji Mkuu wake Neema Msitha jinsi atakavyotekeleza maagizo yake, wakati wa kikao kati ya BMT na TOC tarehe 30 Julai, 2019 Ukumbi wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa Leodeger Tenga akiweka kumbukumbu ya yale ayasemayo Kaimu Mtendaji Mkuu wake Neema Msitha jinsi atakavyotekeleza maagizo yake, wakati wa kikao kati ya BMT na TOC tarehe 30 Julai, 2019 Ukumbi wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

 

Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Leodeger Tenga amefanya mazungumzo na Viongozi wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) kuhusu mambo mbalimbali yatakayosaidia kuimarisha michezo nchini.

Mazungumzo hayo yamefanyika tarehe 30 Julai, 2019 katika moja ya kumbi za Uwanja wa Taifa zilipo Ofisi za BMT baada ya kumwagiza Kaimu Mtendaji Mkuu wake Neema Msitha kuandaa kikao hicho.

Aidha, Mwenyekiti wa BMT kati ya mambo muhimu aliyosisitiza ni kuimarisha uhusiano baina yao kama familia ya michezo sababu itakayosaidia kuwa na lugha moja ya kuyasemea mambo tofauti yatakayopelekea maendeleo ya michezo nchini.

 

Mwenyekiti wa BMT Leodeger Tenga akieleza mikakati ya kuendeleza michezo nchini kwa wajumbe wakati wa kikao chake na TOC
Mwenyekiti wa BMT Leodeger Tenga akieleza mikakati ya kuendeleza michezo nchini kwa wajumbe hawapo kwenye picha wakati wa kikao chake na TOC pamoja na Sekretarieti ya Baraza.

“Lazima tuimarishe uhusiano wetu kwa kuzungumza lugha moja itakayopelekea maendeleo ya michezo nchini,”alisisitiza Tenga na kuongeza kuwa;

“Tuna matatizo mengi kwenye michezo lazima tufanye kazi pamoja ili tulete maendeleo ya michezo,”alisema.

Aliendelea kuwa, lazima tuhakikishe tunakuwa pamoja kuvishauri na kuvisimamia vyama kufuata Sheria na kanuni za Baraza la Michezo la Taifa ikiwemo kuwa na Ofisi zao, akaunti ya kuhifadhia pesa ya chama, kuimarisha Utawala bora pamoja na kuwa na mipango mikakati ya kuleta maendeleo ya mchezo husika.

Viongozi wa TOC, Rais Rashid Gulamu (kulia) Makamu wake Henry Tandau anayefuata, Katibu Mkuu Filbert Bayi anayeeleza jambo na Mjumbe wa Kamati Irene Mwasanga wakiwa makini kusikiliza wakati wa kikao na Mwenyekiti wa BMT Julai 30.
Viongozi wa TOC, Rais Rashid Gulamu (kulia) Makamu wake Henry Tandau anayefuata, Katibu Mkuu Filbert Bayi anayeeleza jambo na Mjumbe wa Kamati Irene Mwasanga wakiwa makini kumsikiliza Katibu wao anachoeleza kwa wajumbe wakati wa kikao na Mwenyekiti wa BMT Julai 30.

Hatahivyo ameahidi kuundwa kamati ya watu wachache katika sehemu tofauti za michezo ikiwemo miundombinu, ufundi na mengine mengi yatakayosaidia maendeleo ya michezo kamati itakayoainisha na kuweka mipango mikakati ya kuivusha michezo hapa ilipo.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mtendaji wa BMT Neema Msitha amemshukuru Mwenyekiti kwa uamuzi wake wa kufanya kikao na wadau hao ambao ndio wanaofanya kazi kwa karibu na baadhi ya vyama vya michezo na kumhakikishia kuwa atashirikiana na TOC kwa karibu kutekeleza maagizo yake.

Katika hatua nyingine Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Filbert Bayi ameeleza kufurahishwa na mwanzo mwema wa mikakati ya Mwenyekiti Tenga na kusema kuwa watampa ushirikiano wa kutosha kuendeleza michezo nchini.

Wajumbe wa Kikao kati ya Mwenyekiti wa BMT Leodeger Tenga na Viongozi wa TOC
Wajumbe wa Kikao kati ya Mwenyekiti wa BMT Leodeger Tenga na Viongozi wa TOC

 

 

 

125 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email4
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2019/07/30/tenga-ateta-na-viongozi-wa-toc-kuhusu-kuimarisha-michezo-nchini/">
RSS