MWAKYEMBE: MPENI USHIRIKIANO MZURI BW. ALVARO KWA AJILI YA FURSA ZAIDI KATIKA MCHEZO WETU WA SOKA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Harrison G. Mwakyembe amewataka viongozi wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) na wadau wa michezo nchini kumpa ushirikiano wa kutosha mwakilishi wa ligi kuu soka nchini Uhispania  maarufu kama La Liga Bw. Alvaro Paya ambaye amechukuwa nafasi ya Bw. Luis Cardenas aliyehamishiwa Falme za kiarabu.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (kulia) akifafanua jambo kwa mjumbe kutoka La Liga nchini Hispania, Alvaro Paya wakati Mjumbe huyo alipomtembelea Waziri Mwakyembe na kujadiliana mambo mbalimbali ya kushirikiana ili kuinua soka la Tanzania.

Mheshimiwa Mwakyembe ameyasema hayo leo tarehe 2 Agosti, 2019 punde tu baada ya kukutana na mwakilishi huyo katika moja ya kumbi za ofisi ya urithi wa ukombozi, ambapo amesema kuna ushirikiano mkubwa sana kati ya Tanzania na Uhispania kupitia mchezo wa mpira wa Miguu jambo ambalo linaleta mafunaa makubwa kwa wachezaji chipukizi nchini.

Mwakilishi wa La Liga nchini Hispania, Alvaro Paya (kushoto) akimwelezea Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe mikakati ya Shirikisho la nchi yake katika kuisadia Tanzania kufanya vizuri katika mchezo wa soka.

“kwa kweli niwaombe sana TFF pamoja na wadau wa mchezo wa soka nchini kumpa ushirikiano mkubwa ndugu yetu Alvaro kwa sababu wameona umuhimu wa nchi yetu katika michezo, utalii na ata amani na kuamua kuendeleza ushirikiano uliopo kati ya viongozi wa Ligi kuu nchini Uhispania na ligi yetu hapa nyumbani na ndio maana wakaamua kumleta mwakilishi mwingine baada ya yule aliyekuwepo kuhamishiwa sehemu nyingine,”alisema Mheshimiwa Mwakyembe.

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi nchini, Boniface Wambura (kushoto) akifafanua kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) mikakati mbalimbali waliyofikia na Mjumbe kutoka La Liga nchini Hispania, Alvaro Paya (hayupo pichani) wakati mjumbe huyo alipomtembelea Waziri Mwakyembe leo jijini Dar es Salaam.

105 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email4
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2019/08/02/mwakyembe-mpeni-ushirikiano-mzuri-bw-alvaro-kwa-ajili-ya-fursa-zaidi-katika-mchezo-wetu-wa-soka/">
RSS