MHESHIMIWA MWAKYEMBE AWATAKA WATANZANIA KUWAUNGA MKONO WAWEKEZAJI ILI KUINUA SOKA KWA PAMOJA

Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison G. Mwakyembe kulia akipata maelezo kutoka mwekezaji wa timu ya Simba Mohamed Dewji (MO) kushoto juu ya ujenzi wa uwanja wa mazoezi wa klabu ya simba uliopo Boko Kinondoni jijini Dar es salaam.
Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison G. Mwakyembe (kulia mwenye suti) akipata maelezo kutoka mwekezaji wa timu ya Simba Mohamed Dewji (MO) (kushoto mwenye suti) baada ya kuzindua jiwe la ujenzi juu ya ujenzi wa uwanja wa mazoezi wa klabu ya simba uliopo Bunju Kinondoni jijini Dar es salaam.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Dkt. Harrison G. Mwakyembe amewataka watanzania kuwaunga mkono wawekezaji ili kuinua soka la Tanzania kwa pamoja ikiwemo  kusaidia katika sehemu tofauti za maendeleo ya michezo kulingana na uwezo wa mtu binafsi ikiwemo hata kutumia nguvu zao wenyewe kama kubeba zege na kazi zingine.

Hayo ameyasema  tarehe 5 Agosti , 2019 katika hafla ya kuzindua jiwe la msingi la ujenzi wa uwanja wa mazoezi  wa klabu ya simba wa ekari 25 uliopo Bunju wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam.

“Hebu basi tuwaunge mkono viongozi  wetu,  kuna kazi ambazo siyo lazima kutoa pesa ikiwemo kubeba zege hebu saidieni ,” alisema Mwakyembe.

Lakini pia Waziri Mwakyembe amempongeza Mwekezaji huyo wa  Simba Mohamed Dewji kwa kuleta chachu na msisimko katika soka la Tanzania na kuwataka watu wengine wenye kupenda maendeleo ya michezo nchini kuiga mfano wake.

“Leo nimeona uwekezaji  wa vitendo  kwa MO hebu watanzania wengine tuige mfano huu ili tulete maendeleo ya michezo nchini,”alieleza.

Waziri Mwakyembe akipewa maelezo na Mwekezaji wa klabu ya simba Mohamed Dewji juu ya uwanja wa mazoezi wa mpira wa miguu alipowasili uwanjani hapo kabla ya kuuzindua rasmi kuendelea na ujenzi
Waziri Mwakyembe katikati suti ya blue akipewa maelezo na Mwekezaji wa klabu ya simba Mohamed Dewji kulia suti ya kushoto juu ya uwanja wa mazoezi wa mpira wa miguu alipowasili uwanjani hapo kabla ya kuuzindua rasmi kuendelea na ujenzi

Aidha,  Dkt. Mwakyembe ameeleza  kuwa nia ya Serikali sio kuuwa soka bali kuendeleza soka kwa kuweka utaratibu utakaofuatwa na vilabu vyote na  wawekezaji  wote lakini isizidi asilimia 49% huku akisisitiza kuwa  soka la leo bila pesa haliwezi kuendelea ambapo alisema kuwa serikali itakuja na kanuni zitakazokubalika na kila mtu.

Aliongeza kuwa, anawataka viongozi wa simba kuleta uwekezaji huo kwa maandishi ili Serikali iutumie kuhamasisha wawekezaji wengine  pamoja na kuleta malalamiko ya ardhi hiyo kwa maandishi ili aweze kumpatia Waziri mwenye dhamana ya ardhi kwa utekelezaji zaidi.

Moja ya kiwanja cha nyasi za asili kilichopo katika uwanja wa klabu ya simba bunju jijini Dar es salaam
Moja ya kiwanja cha nyasi za asili kilichopo katika uwanja wa klabu ya simba bunju jijini Dar es salaam

Hata hivyo Waziri mwenye dhamana ya michezo kwenye hafla hiyo amewataka mashabiki wa simba kutoitumia siku ya simba tarehe 6, 2019 vibaya kuharibu uwanja katika mechi yao maalum ya kuwatambulisha wachezaji wake zidi ya timu ya power Diynamo ya  Zambia kama walivyofanya katika mechi kati yao na Uganda.

Katika hatua nyingine Mwekezaji wa Timu ya Simba Mohamed Dewji  (MO) amesema kuwa, viongozi wa simba wanatarajia kuandaa siku ambayo kila mwanasimba  atachangia na kuonekana ni sehemu ya maendeleo ya simba.

Vilevile ameeleza kuwa, hatapenda kuona simba inachukua tu vikombe vya ushindi bali kuwa katika miundombinu bora.

 

 

 

 

 

140 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email4
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2019/08/05/mheshimiwa-mwakyembe-awataka-watanzania-kuwaunga-mkono-wawekezaji-ili-kuinua-soka-kwa-pamoja/">
RSS