SINGO: UCHACHE WENU MSIJIONE WANYONGE KAPAMBANENI MRUDI NA USHINDI

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Yusuph Singo akimkabidhi bendera Nahodha wa timu ya riadha Gabriel Geay kwa niaba ya wachezaji wanoenda katika michezo ya nchi za Afrika "All African Games'' inayotarajiwa kuanza Agosti 16 nchini Morocco.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Yusuph Singo akitoa nasaha kwa wachezaji baada kumkabidhi bendera Nahodha wa timu ya riadha Gabriel Geay kwa niaba ya wachezaji wanoenda katika michezo ya nchi za Afrika “All African Games”  inayotarajiwa kuanza Agosti 16 nchini Morocco.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Yusuph Singo amewaasa wachezaji wanaoiwakilisha nchi katika michezo ya nchi za Afrika “ALL AFRICAN GAMES” kutojisikia wanyonge kutokana na uchache wao bali wakapambane ipasavyo na kurudi na ushindi katika michezo hiyo.

Rai hiyo ametoa leo Agosti 13, 2019 wakati akiwaaga wachezaji  wa Judo na Riadha na kuwakabidhi bendera ili kwenda kuiwakilisha nchi katika michezo hiyo itakayoshirikisha nchi za Mataifa ya Afrika zipatazo 54 katika michezo zaidi ya 20 inayotarajiwa kufanyika nchini Morocco kuanzia Agosti 16.

Aliendelea kuwa Serikali kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) inaendelea kupambana kutafuta vyanzo vya fedha ili mashindano mengine ya Kimataifa nchi iweze kuwakilishwa na wachezaji wengi zaidi na michezo tofauti.

“Uchache wenu msijione wanyonge nendeni mkapambane ipasavyo mrudi na ushindi, najua mnajua kiu ya watanzania lakini pia Serikali kupitia BMT tunapambana kutafuta vyanzo vya fedha ili mashindano mengine nchi iwakilishwe na wachezaji wengi zaidi,”alisisitiza Singo.

Aidha, Singo aliwasisitiza wachezaji hao kufuata maelekezo ya Walimu wao, kuimarisha ushirikiano na nidhamu vitu ambavyo vitawaletea matokeo mazuri katika mashindano hayo na taifa kwa ujumla.

Tanzania inawakilishwa na michezo miwili (2) katika michezo hiyo ukiwemo mchezo wa Judo unaowakilishwa na wachezaji watatu (3)akiwemo Capt. Abrulrabi Alawi, Sub Cap. Anangisye Pwele, Khamis Hussein na Kocha wao Innocent Malya ambao wanaondoka leo  Agosti 13, huku riadha ikiwakilishwa na wachezaji sita (6)  wakiongozwa Gabriel  Gerald  Geay  bingwa wa mbio za Yiwu chini China atakayekimbia km 5000 na 1500 na Sara Ramadhan.

Wengine Benjamin Kulwa, Ali Khamis Gulam, Regina Mpigachai, Natalia Sulle wakiongozwa na kocha  ambaye pia ni mwanariadha wa zamani Mama Mwinga Mwanjala watakaoondoka awamu ya pili tarehe 21 na kurudi nchini Septemba  1.

Kwa upande wao Manahodha  wa  timu hizo mbili za mchezo wa Judo na Riadha wamewahakikishia watanzania kurudi na ushindi kwa kusema kuwa wamejiandaa vizuri na watafanya vizuri.

Awali Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Neema Msitha alieleza kuwa, taratibu za maandalizi ya timu hizo zimefanyika kwa ushirikiano wa Baraza, Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) pamoja na vyama husika na kusema kuwa watanzania tunatakiwa kuwaombea vijana wetu wafanye vizuri na kuachana na lawama ambazo siyo wakati wake.

Kaimu Katibu Mtendaji BMT Neema Msitha akifafanua jinsi maandalizi ya timu zinazoiwakilisha nchi yalivyofanyika kabla ya timu hizo kukabidhiwa bendera.
Kaimu Katibu Mtendaji BMT Neema Msitha akifafanua jinsi maandalizi ya timu zinazoiwakilisha nchi yalivyofanyika kabla ya timu hizo kukabidhiwa bendera.

79 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email4
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2019/08/13/singo-uchache-wenu-msijione-wanyonge-kapambaneni-mrudi-na-ushindi/">
RSS