MSITHA AWATAKA VIONGOZI WA VYAMA VYA MICHEZO KUIMARISHA UTAWALA BORA ILI KUWAVUTIA WAWEKEZAJI

 Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Neema Msitha (kushoto) akifafanua jambo kwa wachezaji wa mchezo wa vishale (hawapo pichani) kabla ya kuwakabidhi bendera ya Taifa wakielekea nchini Uganda kwenye mashindano ya Afrika Mashariki ya mchezo huo, kulia ni Afisa Michezo toka BMT anayesimamia mchezo huo Bi. Halima Bushiri.

Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT)  Neema Msitha amewataka viongozi wa vyama vya Michezo nchini kuimarisha utawala bora ili kuwavutia wawekezaji kuwekeza katika sekta hiyo na kuifanya michezo kuendelea.

Rai hiyo ameitoa leo tarehe 9 Septemba, 2019  wakati  akiwaaga na kuwakabidhi bendera wachezaji wa mchezo wa vishale nchini kuelekea katika mashindano ya wazi ya nchi za Afrika Mashariki yatakayohusisha nchi nne ikiwemo mwenyeji Uganda, Kenya, Tanzania na Rwanda, mashindano yanayotarajiwa kufanyika kwa siku tatu (3) kuanzia tarehe 13 na kuhitishwa Septemba 15.

Aliendelea kuwa, utawala bora katika michezo unahusisha chama cha mchezo husika kuwa na Ofisi, akaunti ya benki, mashindano  ya ndani yatakayopelekea kupata timu ya Taifa na wachezaji wenye viwango vya kiiwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa pamoja na kuwa mipango mikakati ya muda mfupi na mrefu ya kuendeleza mchezo.

“Kila wakati BMT na mimi binafsi nawasisitiza viongozi wa vyama vya michezo kuimarisha Utawala bora ikiwemo kuwa na Ofisi, akaunti ya kuweka pesa za chama ili kufanya maendeleo ya michezo husika, mipango ya muda mfupi na mrefu pamoja na kuwa na mashindano ya ndani yatakayosaidia kupata  wachezaji wenye viwango wakuiwakilisha nchi katika mashindano mbalimbali ya kimataifa,”alisema na kuongeza kuwa;

“Mkifanya haya yote mtawavutia wawekezaji kuwekeza katika michezo nchini na kuifanya michezo iendelee,” alisisitiza Kaimu Mtendaji wa BMT Neema Msitha.

Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Neema Msitha (kushoto) akimkabidhi nahodha wa timu ya kurusha vishale Bw. Noah Isaya bendera ya Taifa kuiwakilisha nchi kwenye mashindano ya mchezo huo ya Afrika Mashariki yanayofanyika nchini Uganda kuanzia Septemba 13 hadi 15.

Kwa upande wake Nahodha wa timu ya Taifa ya mchezo wa vishale Noah Isaaya ameeleza kuwa wachezaji wamejiandaa vizuri na wanaahidi kuutetea ubingwa wao,  ambapo amesema kuwa Tanzania itawakilishwa na wachezaji zaidi ya thelethini (30) kutoka mikoa tofauti na mashindano hayo yatahusisha timu za taifa, vilabu, mchezaji mmoja mmoja na wachezaji wawili wawili.

Wachezaji wa Tanzania katika mchezo wa vishale wanatarajiwa kusafiri kesho tarehe 10 Septemba, 2019 kuelekea nchini Uganda katika mashindano ya mchezo huo ya nchi za Afrika ya Mashariki yanayotarajiwa kuanza kuanzia tarehe 13 na kumalizika Septemba 15,2019.

Mweka Hazina wa chama cha mchezo vishale Tanzania (TADA), Francis Kabete (kulia) akifafanua jambo kwa Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Neema Msitha (kushoto) kabla ya kukabidhiwa bendera ya Taifa kuiwakilisha nchi kwenye mashindano mchezo ya huo ya Afrika Mashariki yanayofanyika nchini Uganda Septemba 13 hadi 15, katikati ni Afisa Michezo toka BMT anayesimamia mchezo huo Bi. Halima Bushiri.

90 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email4
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2019/09/10/msitha-awataka-viongozi-wa-vyama-vya-michezo-kuimarisha-utawala-bora-ili-kuwavutia-wawekezaji/">
RSS