MHE.MWAKYEMBE: TANZANITE MMEINGIA KATIKA HISTORIA

Waziri mwenye dhamana ya michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na wachezji wa timu ya mpira wa miguu ya wanawake walileta kombe katika mashindano ya nchi ya kusini mwa Afrika yalifanyika Agosti, 2019 nchini Afrika ya kusini
Waziri mwenye dhamana ya michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na wachezji wa timu ya mpira wa miguu ya wanawake (Tanzanite) katika hafla ya kutoa zawadi walioleta kombe katika mashindano ya nchi ya kusini mwa Afrika yaliyofanyika Agosti, 2019 nchini Afrika ya kusini.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison George Mwakyembe ameeleza kuwa Timu ya mpira wa miguu ya Wanawake chini ya umri wa miaka 20 wameingia katika historia kwa kubeba kombe la COSAFA kwa kuichapa Zambia katika fainali ya mashindano ya mpira wa miguu ya wanawake kwa  nchi za kusini mwa Afrika yaliyomalizika Agosti, 2019 nchini Afrika ya Kusini.

Hayo ameyasema tarehe 17 Septemba, 2019 katika hafla iliyoandaliwa na Wizara yenye dhamana ya michezo ya kupata nao chakula pamoja na kuwakabidhi zawadi ya ushindi walioupata katika mashindano hayo.

Aidha, Mhe. Mwakyembe ameeleza kuwa timu hiyo ya tanzanite imefikia kiwango kama cha timu ya umri wa miaka 17 ya vijana wa kiume ya Serengeti Boys.

“Tanzanite mmeingia katika historia na kiwango chenu kimelingana na timu ya vijana ya wanaume ya Serengeti Boys, mmewapiga goli 8 Zambia bila huruma,”Alisema Dkt. Mwakyembe.

 

Wachezaji wa timu ya wanawake katika hafla ya kupata chakula na viongozi wenye dhamana ya michezo pamoja kukabidhiwa zawadi baada ya kutwaa ubingwa wa mashindano ya COSAFA Afrika ya Kusini hafla iliyofanyika Serena Hoteli jijini Dar es salaam.
Wachezaji wa timu ya wanawake katika hafla ya kupata chakula na viongozi wenye dhamana ya michezo pamoja kukabidhiwa zawadi baada ya kutwaa ubingwa wa mashindano ya COSAFA Afrika ya Kusini hafla iliyofanyika Serena Hoteli jijini Dar es salaam.

“Nina imani kubwa na nyie kina mama soka lenu linaenda vizuri hata U 20 yenu nina uhakika mtaenda vizuri na mnahamasa kubwa, wawekezaji wekezeni kwa hawa tutafika mbali sana hatukamatiki,”alisema na kuongeza kuwa;

“Mmetufanyia mazuri sana, mmetufanya tucheke, tufurahi na tujisikie vizuri sana kwa mara ya kwanza katika historia ya soka nchini, soka siyo la wanaume tu nyie mmethibitisha hilo, wasikilizeni walimu wenu soka ni ajira ya uhakika na afya ”alisisitiza.

Waz

Waziri mwenye dhamana ya michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akikabidhi zawadi kwa Nahodha wa Tanzanite Queens Enekia Kasonga

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa TFF Alfredy Kidau alieleza mipango ya Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) kuendeleza vipaji vya vijana wote wakiwemo wa kike kwa kuibua vipaji hivyo mashuleni.

Katika hatua nyingine Nahodha wa timu ya mpira wa miguu ya wanawake chini ya umri wa miaka 20 ameeleza kufurahishwa na hatua ya Serikali kufurahishwa na hatua waliofikia na kuahidi kuwa imewatia hamasa ya kufanya vizuri zaidi.

Awali Katibu Mkuu wa Wizara yenye dhamana ya michezo Susan Mlawi ameeleza kufurahishwa sana na vijana wa kike wa mpira wa miguu na kusema kuwa katika awamu yake wameleta makombe matatu huku akiahidi kuendelea kuwa nao pamoja kwa hali na mali.

 

 

61 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email4
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2019/09/18/mhe-mwakyembe-tanzanite-mmeingia-katika-historia/">
RSS