NEEMA: JUHUDI ZA KUIFANYA MICHEZO YA JADI KUTAMBULIKA NI ZA CHAMA HUSIKA

IMG_3578Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bi. Neema Msitha amesema mchezo wa jadi wa mieleka unatambulika nchini kupitia chama cha michezo ya Jadi Tanzania (CHAMIJATA) kilichosajiliwa na BMT kupitia ofisi ya msajili wa vyama vya michezo, hivyo juhudi ya kuufanya mchezo huo kutambulika zinatakiwa kufanywa na chama husika.

Bi. Neema ameyasema hayo leo tarehe 24 Septemba, 2019 alipokuwa anajibu swali la mtangazaji wa kituo cha TBC Evans Muhando aliyehoji ni kwa nini mchezo wa mieleka hautambuliki? Baada ya kuhudhuria Tamasha la Utamaduni kanda ya Afrika Mashariki JAMAFEST kwa upande wa michezo ya jadi iliyofanyika katika uwanja wa uhuru jijini Dar es Salaam.

IMG_3544“mchezo huu unatambulika na ndio maana umesajiliwa, sisi kama Baraza la michezo la Taifa tuna chama kinaitwa Chama cha michezo ya Jadi ,lakini juhudi za kuufanya utambulike ni juhudi za chama ndio maana sisi kukiwa na matamasha kama haya kama serikali tunajiongeza kuwaita waje waonyeshe, ila wanapaswa wajiongeze kuusambaza kwa kuandaa matamasha wilayani na mikoani ili uweze kutambulika zaidi,” alisema Neema.

Aidha Neema amewataka wazazi na walezi nchini kuwapa nafasi watoto wacheze michezo ya jadi, ambayo inaimarisha afya zao kupitia mazoezi wanayofanya sanjari na ulinzi binafsi kwani inawafanya vijana kuwa na nguvu sanjari na kuwa na mbinu mbalimbali za kujilinda.

IMG_3404Kwa upande wake mchezaji wa mchezo wa mieleka Hassan Kizara amesema ili kuhakikisha mchezo huo unafahamika inabidi kuwe na uhamasishaji wa hali ya juu kwa kufundishwa mashuleni pamoja na kwenye vikundi vya mitaani.

“kwa kweli uhamasishaji ni mdogo sana kwa upande wa mchezo wa mieleka inabidi mchezo huu uweze kufundishwa mashuleni pamoja na mitaani kwenye vikundi vya vijana ili uweze kufahamika zaidi,” alisema Hassan.

60 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email4
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2019/09/24/neema-juhudi-za-kuifanya-michezo-ya-jadi-kutambulika-ni-za-chama-husika/">
RSS