WAZIRI MKUU ASAIDIA TaBSA KUFAIDIKA

Kaimu Msajili wa vyama vya michezo nchini Benson Chacha (wapili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe kutoka kituo cha mchezo wa Baseball nchini Marekani wakwanza kushoto Duncan Webb alipofanya ziara Ofisi za BMT kufanya mazungumzo namna kituo chao kitakavyosaidia mchezo huo nchini.
Kaimu Msajili wa vyama vya michezo nchini Benson Chacha (wapili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja baada ya mazungumzo  na ujumbe kutoka kituo cha mchezo wa Baseball nchini Marekani wa kwanza kushoto Duncan Webb alipofanya ziara Ofisi za BMT na Katibu wa TaBSA Alpherio Nchimbi (katikati), mtoto wa Mwanzilishi na mchezaji David Robinson kulia, kufanya mazungumzo namna kituo chao kitakavyosaidia mchezo huo nchini.

Waziri Mkuu wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesaidia Chama cha Mchezo wa Baseball na Softball Tanzania (TaBSA) kupata ufadhili wa fursa tofauti za maendeleo ya mchezo huo kutoka Kituo cha mchezo huo cha Marekani kijulikanacho kwa jina la ‘Los Angeles Dodgers’ ujumbe uliofika jana katika Ofisi za Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kupitia Uongozi  wa chama cha mchezo huo nchini.

Fursa hiyo imepatikana baada ya Waziri Mkuu kuiita familia ya aliyekuwa  Mwanzilishi na Mchezaji  mahiri  wa mchezo huo nchini Marekani  (Jack Robinson) ambao kwa sasa wanaishi nchini Tanzania ambapo, aliwataka kufanya  jitihada za kuitangaza Tanzania kupitia kituo cha mchezo huo nchini humo kinachomilikiwa na familia ya mchezaji huyo ili kusaidia kuuendeleza mchezo huo nchini.

Kikao cha mazungumzo kati ya BMT, TaBSA na ujumbe kutoka Los Angeles kuhusu ushirikiano wa maendeleo ya mchezo wa Baseball nchini tarehe 25 Septemba,2019
Kikao cha mazungumzo kati ya BMT, TaBSA na ujumbe kutoka Los Angeles kuhusu ushirikiano wa maendeleo ya mchezo wa Baseball nchini tarehe 25 Septemba,2019

Aidha, kupitia rai hiyo ya Waziri Mkuu,  mtoto wa mchezaji huyo David Robinson ameandaa ziara ya kwanza ya mmoja ya wana Los ngeles  Dodgers  kuja nchini na kukutana na viongozi wa mchezo huo pamoja na Serikali kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ambapo walifanya mazungumzo ya namna watakavyosaidia mchezo huo nchini tarehe 25 Septemba,2019.

Kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa BMT Kaimu Msajili wa Vyama vya Michezo Benson Chacha alieleza kufurahishwa na ujio wa ujumbe huo na kuwaeleza maeneo mbalimbali ya kusaidia katika mchezo huo ikiwemo vifaa, miundombinu pamoja na wataalamu na kuwaomba wasaidiae pale wanapoona inafaa lakini pia waangalie fursa za kuwekeza na katika michezo mingine pia kama wanauwezo huo.

 

Mazungumzo yakiendelea
                              Mazungumzo yakiendelea

Lakini pia alimtaka Katibu wa TaBSA Alpherio Nchimbi pamoja Duncan Webb kufuata taratibu zote za nchi ikiwemo kuandikishana mikataba pamoja na wataalamu kuwa na vibali vya kufanya kazi  nchini, lakini pia kufanya mawasiliano mapema wanapotaka kuleta vifaa nchini ili taratibu ziwekwe mapema kuondoa vikwazo vya kuitoa bandarini.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Rasilimali kutoka Los Angeles Dodgers Duncan Webb  alieleza  kuwa, kituo chao kitashirikiana na TaBSA kuuendeleza mchezo huo nchini katika sehemu tofauti na kwa  awamu tofauti ikiwemo kusaidia vifaa na wataalamu wa kufundisha, na kueleza kuwa awamu ya kwanza itakuwa Desemba mwaka huu.

65 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email4
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2019/09/26/waziri-mkuu-asaidia-tabsa-kufaidika/">
RSS