DOKTA ALLY POSSI: NAAMINI KUWA MTAFANYA VIZURI KWENYE MASHINDANO YA AFRIKA.

IMG_3916Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Ally Possi amewataka wachezaji wa Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu kwa watu wenye ulemavu, kuipeperusha vyema bendera ya Taifa la Tanzania katika mashindano ya Afrika yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi tarehe 1 Oktoba, 2019 nchini Angola.

Dkt. Possi ameyasema hayo leo tarehe 30 Septemba, 2019 alipokuwa anaiaga na kuikabidhi bendera timu hiyo, tukio lililofanyika katika moja ya kumbi za uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa anaimani kubwa na timu hiyo kufanya vizuri katika mashindano hayo na itakaporejea nchini, itapagwa mikakati kabambe kuhakikisha michezo yote ya walemavu inafanya vizuri na kupiga hatua.

“mnabeba bendera ya Taifa ambayo ni jukumu kubwa na ni jukumu la kitaifa naamini mtapeperusha bendera ya Taifa vizuri, lakini la pili ambalo ni kubwa zaidi naomba tutumie mashindano hayo kama fursa na naamini mtafanya vizuri na mkirudi na ushindi tutakaa pamoja kuhainisha njia za kuboresha michezo yote ya walemavu nchini,”alisema Dkt. Possi.

Aidha Dkt. Possi amesema mchezo wa mpira wa miguu ni fursa ya ajira ambayo inazalisha ajira mbalimbali kwa sababu kupitia mpira wa miguu serikali inapata kodi, lakini pia hata wachezaji wanatengeneza ajira kwa watu wengine wanaowazunguka kama wajenzi na kadhalika.

 

62 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email4
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2019/09/30/dokta-ally-possi-naamini-kuwa-mtafanya-vizuri-kwenye-mashindano-ya-afrika/">
RSS