DOKTA TULIA ALITAKA BMT KUSAKA VIPAJI VYA RIADHA MIKOANI

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dokta Tulia Ackson, amelitaka Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuhudhuria mashindano ya Riadha yanayofanyika katika mikoa mbalimbali nchini, ili kuweza kusaka vipaji vya Riadha.

IMG_9529Mheshimiwa Tulia ameyasema hayo leo tarehe 7 Disemba, 2019 alipokuwa anafungua mashindano ya riadha kwa wanawake yajulikanayo kama Ladies First yanayofanyika katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kwa mara ya Tatu mfululizo kwa kushirikisha wanariadha kutoka mikoa 27 ya Tanzania Bara na Visiwani.

IMG_9405“Baraza letu la Michezo la Taifa watusaidie, kwa sababu hii michezo inafanyika sehemu mbalimbali, hawa sawa wamepata fursa ya kuja hapa ni kwa idadi ambayo imetajwa pengine mikoa mingine, kama msingesema ni kwa idadi ya watu watano wangeleta watu zaidi, kwa hiyo ni zoezi ambalo mtusaidie mashindano yanayofanyika katika ngazi ya wilaya na mikoa, mjaribu kwenda huko kwa sababu vipaji mnaweza mkaviona vya watoto hawa wakiwa kule, kuliko wakija hapa ambao tayari wameshachaguliwa, wako ambao wanaweza kuwa hawajaja kwa sababu ya idadi iliyotajwa, lakini pengine uwezo wao ni mkubwa zaidi,”alisema Dokta Tulia.

15 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email4
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2019/12/07/dokta-tulia-alitaka-bmt-kusaka-vipaji-vya-riadha-mikoani/">
RSS