HONGERA NAHODHA MBWANA SAMATTA (DIEGO)

Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Bi. Neema Msitha amempongeza mshambuliaji na nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Mbwana Samatta kwa jitihada alizozionyesha katika kusakata kabumbu na kufanikiwa kusajiliwa na klabu ya Aston Villa inayoshiriki Ligi Kuu nchini Uingereza almaarufu kama EPL.

SamaBi. Neema ametoa pongezi hizo leo tarehe 21 Januari, 2020 alipokuwa anazungumza na chombo cha Habari cha Star Tv, Ofisini kwake uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambapo amesema Tanzania inajivunia Samatta kwa kuwa mchezaji wa kwanza kutoka nchini kucheza Ligi kubwa Duniani EPL.

“kama BMT kwa kabisa tunampongeza sana kijana wetu Samatta kwa juhudi ambazo amezionyesha kuanzia akiwa na klabu ya Simba, Tp Mazembe, KRC Genk na sasa amejiunga na Aston Villa, ni matumaini yangu kuwa, vijana wengine wataiga mfano wake na kuwa nyota wazuri katika mchezo wa mpira wa miguu,”alisema Neema.

Aidha Bi. Neema amewataka wazazi nchini kuwapa fursa watoto kuonyesha vipaji vyao katika fani mbalimbali ikiwemo michezo, kwani kwa kufanya hivyo watanufaika sana kwa kuwa michezo ni Afya na ni Ajira pia.

83 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email4
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2020/01/21/hongera-nahodha-mbwana-samatta-diego/">
RSS