Coastal Yaanza Vizuri Michuano ya Kombe la Uhai

Coastal yaanza vizuri michuano ya kombe la Uhai

 Coastal Union ya Tanga imeanza vizuri michuano ya kuwania Kombe la Uhai inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom baada ya kuifunga Tanzania Prisons mabao 2-1. Mechi hiyo ya kundi A imechezwa leo asubuhi (Desemba 11 mwaka huu) Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.

Coastal Union ilimaliza kipindi cha kwanza ikiwa tayari imepachika mabao hayo yaliyofungwa dakika ya 24 na 33 kupitia kwa Ramadhan Same na Yusuf Chuma. Tanzania Prisons ambayo itacheza mechi yake pili kesho jioni (Desemba 12 mwaka huu) Uwanja wa Azam ulioko Chamazi dhidi ya JKT Ruvu ilipata bao lake dakika moja kabla ya filimbi ya mwisho.

Mechi nyingine za kesho ni Toto Africans dhidi ya Coastal Union itakayochezwa saa 2 asubuhi Uwanja wa Azam. Katika kundi B, Simba na African Lyon zitaoneshana kazi asubuhi Uwanja wa Karume wakati Azam na Polisi Morogoro zitacheza saa 10 jioni kwenye uwanja huo huo. Kundi C kesho ni Kagera Sugar vs Oljoro JKT saa 2 asubuhi Uwanja wa Karume, na Yanga na Ruvu Shooting zitaumana saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Azam. Kutoka: Tovuti ya TFF

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *