Taifa Queens Return in Triumph

Timu ya taifa ya Netiboli ya Tanzania ‘Taifa Queens’
Timu ya taifa ya Netiboli ya Tanzania ‘Taifa Queens’  – December 2012

Timu ya taifa ya Netiboli ya Tanzania ‘Taifa Queens’ imerejea kwa kishindo leo baada ya kushiriki na kutwaa      Kombe la michuano ya Kimataifa iliyokuwa ikifanyikia Singapore barani Asia. Taifa Queens ilitwaaa ubingwa huo    baada ya kuingia fainali ikiwa na pointi 10 ikicheza na timu ya Malasia iliyokuwa na pointi 4 ambapo ilifanikiwa    kuifunga magoli 45-38.

Akizungumza baada ya kurejea, Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA), Anna Bayi alisema maandalizi ni kitu kizuri sana, anaamini kocha aliwapa wachezaji mbinu za kutosha hadi kupelekea ubingwa huo.      “Hii imetusaidia sana maana kocha mwenyewe ni kijana hivyo anambinu za kisasa kitu kilichotusaidia wakati tukiwa ugenini, hakuna kitu kizuri kama kupigiwa wimbo wa taifa lako ukiwa ugenini huku wazungu ambao ni wenyeji wa mashindano hayo wakiwa penbeni,” alisema Bayi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *