Michezo Kwa Jamii

MICHEZO KWA JAMII

Michezo kwa jamii ni moja ya mpango wa Baraza la Michezo  katika kuinua ushiriki wa jamii katika michezo kutoka ngazi ya Kijiji, Wilaya, Mkoa  hadi Taifa.

Kwa mujibu wa Wizara ya Habari,Vijana Utamaduni na Michezo, Michezo kwa jamii ni jukumu la Baraza la Michezo la Taifa kwa kushirikiana na Mamlaka za Mitaa za Wilaya na Manispaa.

Mpango huu ulizinduliwa kisheria tarehe 11th August,2017  na aliyekuwa Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mr. Joel Bendera  wilayani Kondoa, Dodoma. Wakati wa Uzinduzi zilikuwepo Kamati chache za michezo kutoka Kondoa Mjini ambazo zilipewa mafunzo kuhusu sheria,kanuni na majukumu ya michezo.  Hii inadhihirisha kuwa watu wanahitaji kupewa elimu kuhusu  michezo.

UDSM TACLKLE 2

 

 

 

 

 

 

 

 

LENGO NA DHAMIRA YA MICHEZO  KWA JAMII

Kuanzishwa kwa michezo kwa jamii kumetokana na kutopewa  kipau mbele tasnia ya michezo, vilevile watu hawahamasishwi kushiriki. Ambapo unahitajika ushawishi wa jamii katika ngazi na nafasi zote kushiriki katika michezo. Michezo kwa jamii kama Mpango na lengo la kutimiza dhamira hii ni:-

  • Kutoa ujuzi wa uongozi wa michezo, sheria, na kanuni za mpira wa miguu, mpira wa mikono, mbio, na michezo mingine. Vilevile kutoa elimu kuhusu masuala mtambuka mfano;Ukimwi na mazingira.
  • Kuandaa wataalamu wa michezo ambao watasaidia kutoa mafunzo ya michezo mashuleni,vyuoni na vyuo vikuu.
  • Kusimama kama chombo cha kutoa elimu vijijini na  wilayani  kwani, Baraza peke yake haliwezi kukidhi malengo ya Taifa.
  • Kutoa vifaa vya michezo  kwa kijiji au kata kwa lengo la kuinua vipaji vya vijana katika michezo.
  • Kuwajengea walimu wa shule za msingi misingi ya kuhusisha haiba na michezo katika ufundishaji wa masomo kila siku.
  • Kutoa elimu kwa walimu jinsi ya kupanga na kuandaa maeneo ya michezo kwa kuzingatia vipimo vinavyotakiwa (50m to 100m) na muelekeo (Kaskazini – Kusini)
Washiriki wa mpira wa wavu mara baada ya kugawiwa vifaa
Washiriki wa mpira wa wavu mara
baada ya kugawiwa vifaa

 

 Mwanza4

 

 

   

175 total views, 1 views today

Follow by EmailO
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/michezo-sports/michezo-kwa-jamii-2/">
RSS