Miradi

1. International  Inspiration

Serikali ya Tanzania inatekeleza mradi wa “International Inspiration” ambao lengo lake kuu ni kuboresha maisha ya watoto na vijana kupitia michezo.

Mradi huu ni matokeo ya ahadi iliyotolewa na Nchi ya Uingereza huko Singapore katika mchakato wa kuomba kuwa mwenyeji wa michezo ya Olimpiki 2012. Wadau wakuu katika kutekeleza mradi huu hapa Tanzania ni:

Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (WHVUM), Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (WEMU), Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto (WMJJW), Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM TAMISEMI), Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) na Kamati ya Paralimpiki Tanzania (TPC). Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwa niaba ya Serikali ya Tanzania limekuwa likiratibu mradi huu likishirikiana na wadau na washirika wa maendeleo mbalimbali katika kuleta mafanikio ya sekta ya michezo nchini.Washirika wakuu wa maendeleo wa mradi huu kwa Tanzania ni:-

UK Sport International, British Council, TOP Foundation, na Laureus Sport for good.

2. Tanzania Beck-with International Leadership Development Programme                                                 (BILD Tanzania)

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwa niaba ya Serikali ya Tanzania limekuwa likishirikiana na wadau na washirika wa maendeleo mbalimbali katika kuleta mafanikio ya sekta ya michezo nchini.

Moja kati ya juhudi hizi ni mradi wa Uongozi kupitia Michezo kwa Vijana ambao kwa kifupi unajulikana kama BILD Tanzania. Mradi huu ulitekelezwa kwa ushirikiano wa BMT na TOP Foundation ya Uingereza kupitia UK Sport International. Mradi huu uliitwa Beckwith ili kumuenzi Sir John Beckwith mwenyekiti wa TOP Foundation waliofadhili mradi huu.

BILD Tanzania Evaluation Report

309 total views, 1 views today

Leave a Reply

Follow by Email4
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/michezo-sports/miradi-projects/">
RSS