International Inspiration

Serikali ya Tanzania inatekeleza mradi wa “International Inspiration” ambao lengo lake kuu ni kuboresha maisha ya watoto na vijana kupitia michezo.

Mradi huu ni matokeo ya ahadi iliyotolewa na Nchi ya Uingereza huko Singapore katika mchakato wa kuomba kuwa mwenyeji wa michezo ya Olimpiki 2012. Wadau wakuu katika kutekeleza mradi huu hapa Tanzania ni:

 • Baraza la Michezo la Taifa (BMT),
 • Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (WHVUM),
 • Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (WEMU),
 • Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto (WMJJW),
 • Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM TAMISEMI),
 • Taasisi ya Elimu Tanzania (TET),
 • Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) na
 • Kamati ya Paralimpiki Tanzania (TPC).

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwa niaba ya Serikali ya Tanzania limekuwa likiratibu mradi huu likishirikiana na wadau na washirika wa maendeleo mbalimbali katika kuleta mafanikio ya sekta ya michezo nchini.

Washirika wakuu wa maendeleo wa mradi huu  kwa Tanzania ni

 • UK Sport International,
 • British Council,
 • TOP Foundation, na
 • Laureus Sport for good.

Kwa taarifa zaidi soma taarifa za mradi huu zitakazoambatishwa hapa.

II LogoLaureus Sport For GoodUKSPORTDS

382 total views, 2 views today

Leave a Reply

Follow by Email4
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/michezo-sports/miradi-projects/international-inspiration/">
RSS