Usajili na Uchaguzi

UONGOZI NA CHAGUZI ZA VYAMA VYA MICHEZO 

  1. Utangulizi
  2. Kazi za Baraza
  3. Kanuni za Usajili wa Chama ch Michezo
  4. Utaratibu wa Kusajili Kilabu au Chama
  1. UTANGULIZI

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) liliundwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Sheria Na.12 ya Mwaka 1967 na Marekebisho yake Na. 6 ya 1971 ya Baraza la Michezo la Taifa Pamoja na Kanuni za Baraza la Michezo la Taifa na Kanuni za Usajili Na. 442 za Mwaka 1999.

KAZI ZA BARAZA LA MICHEZO LA TAIFA

i  Kuendeleza, Kustawisha na kudhibiti aina Zote za Michezo ya ridhaa Kitaifa kwa Ushirikiano na Vyama au Vikundi vya Michezo vya ridhaa kwa kutoa:

ii  Kuhimiza na Kutoa fursa za ushirikiano miongoni mwa vyama mbalimbali vya Taifa.

iii  Kuidhinisha mashindano ya kitaifa na ya kimataifa katika michezo na tamasha vilivyoandaliwa na vyama vya kitaifa na vyama vingine.

iv  Kuandaa, baada ya kushauriana na vyama vya kitaifa vinavyohusika, mashindano na tamasha vya kitaifa na kimataifa kwa nia ya kubadilishana uzoefu na kukuza mahusiano ya kirafiki na mataifa mengine.

v  Kuamsha ari ya kupenda aina zote za michezo kwa ngazi zote.

Katika kutekeleza majukumu yake kulingana na matakwa ya sheria, Baraza la Michezo linasimamia chaguzi za vyama vya michezo

Leave a Reply

Follow by Email
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/usajili/">
RSS