Utaratibu wa Kusajili Kilabu au Chama

UTARATIBU WA KUSAJILI KILABU / CHAMA CHA MICHEZO TANZANIA

(1) Chama chochote kinachotaka kusajiliwa kitapeleka maombi yake kwa Msajili Msaidizi aliyeko katika wilaya ambayo ni makao makuu ya chama hicho. Maombi haya yaambatanishwe na:

a) Muhtasari wa kikao cha wanachama kilichofikia uamuzi wa kuunda chama na kupitisha  Katiba;

b) Nakala tatu za Katiba ya chama;

c) Nakala tatu za kanuni za fedha za chama;

d) Nakala tatu za kanuni za uendeshaji shughuli za chama;

e) Orodha ya majina ya uanachama wake na namba ya uanachama kwa msajili

(2) Baada ya kuwasilishwa maombi .msajili msaidizi atawapatia viongozi wa chama fomu  Na. BMT 1 na BMT 2 wazijaze na kisha Msajili wa Vyama vya Michezo

(3) Msajili akishayapokea maombi hayo, atayahakiki na endapo hataona upungufu wowote, atakisajili chama hicho kwa kufanya yafuatayo:

a) Kuingiza jina la chama katika daftari la usajili wa Vyama vya Michezo; na
b) Kutoa hati ya Usajili.

(4) Endapo Msajili atabaini upungufu kwenye maombi yaliyowasilishwa kwake na Msajili Msaidizi, atawajulisha wahusika upungufu uliopo kwa kutumia fomu Na. BMT 3 ili wakafanyie marekebisho.

(5) Endapo msajili atakataa kukisajili chama, atatoa taarifa kwa chama husika kwa kutumia         Fomu Na .4 BMT

(6) Chama cha mchezo wowote hakitaruhusiwa kuendesha shughuli za Michezo bila kusajiliwa. Aidha, chama kilichosajiliwa hakiruhusiwi kuwa na ushirikiano wa kimichezo na chama ambacho hakijasajiliwa.

4. (1) Kila katiba ya chama inatakiwa kuonyesha kwa uwazi mamboyafuatayo:

a) Jina la Chama

b) Anuani kamili, ikiwa na mate au kijiji, namba ya nyumba au ofisi, namba ya sanduku la Posta na Simu kama ipo na pia Mji, Wilaya na Mkoa.

c) Madhumuni.

d) Idadi na aina ya michezo

e) Muundo wa chama

f) Wajibu na kazi za kamati mbalimbali.

g) wajibu na kazi za viongozi na Wanachama

h) Kalenda ya :

i.)      Mikutano ya kamati ndogondogo;

ii.)    Mikutano ya kamati ya Utendaji;

iii.)  Mkutano Mkuu wa uchaguzi

iv.) Taratibu za kushughulikia migogoro na rufaa;

j) Sifa za wagombea uongozi zimewekwa bayana kulingana na aina ya mchezo, utaalam, uzoefu, kiwango cha elimu na ngazi ya chama husika kwa mujibu wa sera ya maendeleo ya michezo.

101 total views, 2 views today

Leave a Reply

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/usajili/utaratibu-wa-kusajili-kilabu-au-chama/">
RSS